Loading...

Kadinali wa kanisa katoliki akutwa na hatia ya unyanyasaji watoto kingono


Kadinali George Pell wa kanisa katoliki nchini Australia amekutwa na hatia za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, hii inamfanya kuwa kiongozi wa hadhi ya juu kabisa wa Kanisa kukutwa na hatia hii.

Pell aliwafanyia unyanyasaji vijana wawili mwaka 1996, lakini amekana kuhusika.

Mashataka yalifunguliwa tangu mwezi December lakini huenda hayakuwekwa wazi kutokana na sababu za kisheria.

Pell mwenye umri wa miaka 77 anatarijiwa kuhukumiwa siku ya Jumatano, lakini mawakili wake wanasema kua watakata rufaa hatia hiyo.

Kiongozi huyu wa kanisa aliyekua anashikilia nafasi ya Muweka hazina, na ni miongoni mwa viongozi wenye nguvu Zaidi kanisani,

Kesi yake ilisikilizwa mara mbili mwaka jana,

Amekutwa na hatia, ikiwemo ya kumuingilia mtoto chini ya miaka 16, na hatia zingine nne za kuwafanyia vitendo visivyo vya kawaida watoto wa chini ya miaka 16.

Kanisa katoliki duniani kote kwa miaka ya hivi karibuni, limekubwa na kashfa ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, na kudaiwa kuwa wamekua wakificha masuala hayo.

Kwa wakati wote kadinali Pell amekanusha kuhusika na matukio yote , kwa sasa yupo katika mapumziko marefu wakati wote wa kesi hii ikiendelea.

Mahakama ilisikiliza nini?

Pell alikua katika mwaka wake wa kwanza katika kanisa huko Melbourne mwaka 1996 alipowafanyia unyanyasaji watoto , baada ya kuwaambia kuwa walikunywa mvinyo wa kanisa, aliwalazimisha kumfanyia vitendo visivyofaa kama adhabu yao.

Kanisa lilipata fursa ya kusikia ushahidi kutoka kwa mmoja wa wahanga wa unyayasaji huo, muathiriwa mwingine tayari amekufa.

Hatia za Pell sasa zimevutia umakini wa wetu wengi ikizingatiwa , Papa Francis ameanza jitihada za kupambana na tatizo hili ikiwemo mkutano uliofanyika wiki iliyopita.

Papa alisema nini hasa?
Kadinali Pell akiwa pamoja na papa, picha iliyopigwa mwaka 2015
"Nakumbushwa matendo ya kikatili katika majaribio ya kidini ,wakati mmoja yataenea kwenye utamaduni fulani,wa kutoa kafara binadamu -hasahasa watoto -katika Ibaada za wapagani" Alisema wakati akimaliza siku nne katika kongamano lililofanyika Vatican.

"Unyama unaotendeka kote ulimwenguni unaweza kuja kua wa hali ya juu na kulikashifu kanisa, kwasababu tu ya kulinganishwa na mamlaka ya kimaadili na uaminifu

Alipochaguliwa mwaka 2013, Alifanya "Maamuzi ya Kihatua" kuhusiana na unyanyasaji wa kingono unaohusisha watawa ,Anasema bado hatua za kutosha hazijachukuliwa kuwashikilia watawa watakaohusishwa na unyanyasaji.

Maelfu ya watu huenda wakawa wamefanyiwa unyanyasaji wa kingono na watawa kwa miongo mingi sasa ,Na kanisa limekua mara zote likishutumiwa kufunika uhalifu huo kote ulimwenguni

Papa Francis yupo katika wakati mgumu kuweza kuweka uongozi na kuzalisha suluhu itakayoleta muafaka juu ya mgogoro mkubwa unaokumba kanisa -Huku wengine wakisema limepoteza mamlaka yake ya kimaadili na kua katika hali mbaya.

Chanzo: BBC
Kadinali wa kanisa katoliki akutwa na hatia ya unyanyasaji watoto kingono Kadinali wa kanisa katoliki akutwa na hatia ya unyanyasaji watoto kingono Reviewed by Zero Degree on 2/26/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.