Loading...

Ramsey huyoo Ligi Kuu ya Italia


Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu ya Juventus msimu ujao kwa katika cha pauni 400,000 kwa wiki.

Nyota huyo wa miaka 28 amekubali mkataba wa miaka minne utakaomwezesha kujiunga na Mabingwa wa Ligi Kuu ya Italia bila malipo baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 11.

Ramsey alifuzu sehemu ya kwanza ya uchunguzi wa kimatibabu mwezi Januari, na kuchagua Juve baada ya kushauriana na wadau kadhaa wa klabu hiyo.

Mkataba wake unaisha Juni 30 na Gunners hawatapokea malipo yoyote atakapo ondoka, ambapo atakuwa mchezaji kutoka Ligi Kuu ya Uingereza anayelipwa mshahara mkubwa.

Ikithibitisha mpango huo, Juventus imesema italipa ada ya pauni milioni 3.2 lakini haikuelezea ada hiyo ni ya nini.

Arsenal imesema mchango wa Ramsey ulikuwa mkubwa sana katika klabu hiyo na kuongeza kuwa "atasalia katika kumbu kumbu ya historia" ya mashabiki.

Akiandika katika mtandao wake Instagram, Ramsey aliwashukuru mashabiki wa Arsenal na kusema kuwa"ataendelea kuwaunga mkono kwa asilimia mia moja".

Aliendelea kuandika : "Mlinikaribisha katika klabu hiyo nikiwa kijana mdogo na nimeshuhudia nyakati nzuri na mbaya.

"Nasikitika kuondoka baada ya miaka 11 ya ufanisi sijui nielezee vipi hisia zangu muda huu. Asanteni." Charles, Rush, Ramsey...

Tovuti ya Juventus imemkaribisha Ramsey kwa kuandika kwamba atakuwa mkazi wa Wales wa tatu kuiwakilisha klabu hiyo baada ya John Charles na Ian Rush.

Ramsey, alijiunga na Arsenal akitokea Cardiff City mwaka 2008 kwa ada ya £4.8m, pia aliwahi kufanya mazungumzo na Barcelona na kupokea ofa kutoka klabu ya Paris St-Germain.

Bayern Munich, Inter Milan na Real Madrid walionesha nia ya kutaka kumnunua kiungo huyo, huku mshambuliaji wa Real Gareth Bale akidaiwa kumshauri kuungana nae katika ligi kuu ya Uhispania.


Arsenal ilimpatia Ramsey ofa ya mkataba mpya mwezi Septemba lakini hatua hiyo ilipingwa na wakuu wa klabu ambao hawakuwa tayari kugharamia mshahara wake mkubwa na pia kocha mkuu Unai Emery kutilia shaka jukumu lalake kikosini, ambapo Ramsey alitaka kucheza namba nane kitu ambacho kilikuwa kinakinzana na maono ya Emery.

Amechezea Arsenal mara 259, na kufunga mabao mara 61.
Ramsey huyoo Ligi Kuu ya Italia Ramsey huyoo Ligi Kuu ya Italia Reviewed by Zero Degree on 2/12/2019 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.