Loading...

Ethiopian Airline yaua abiria 149 na wafanyakazi 8


Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.

Taarifa ya Shirika la Ndege la Ethiopia imesema kuwa abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege ya shirika hilo iliyopata ajali wote wamefariki.

Takriban wasafiri 149 na wahudumu wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hakuna hata mmoja aliyeweza kunusurika na wote wamekufa, aliliambia shirika la habari la kitaifa la Ethiopia msemaji wa Ethiopian Airlines.

Mkurugenzi Mkuu wa Ethiopian Airlines akiwa katika eneo la tukio la ajali.

Mkurugenzi mtendaji wa Ethiopian Airlines CEO Tewolde Gebremariam ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba miongoni mwa waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na :

Wakenya 32, raia wa Canada 18, raia tisa wa Ethiopia, wataliano 8, Wachina 4, wamarekani 4, waingereza 7, Wafaransa 7, Wamisri 6, Wajerumani 5, Wahindi 4 na wanne kutoka Slovakia.

Waastralia 3, Waswis 3, Warusi 3, Wakomoro 2, Wahispania 2, Wapoland 2, Waisraeli 2.

Kulikuwa pia abiria mmoja mmoja kutoka nchi za ubelgiji, Indonesia, Somalia, Norway, Serbia, togo, Msumbiji, rwandsa, Sudan, Uganda na Yemen.

Afisa wa itifaki wa Somalia ameripotiwa kuwa mmoja wa watu waliokufa kwenye ajali hiyo , kulingana na kituo cha kibinafsi cha Radio Dalsan, kinachomilikiwa na redio ya Somalia.
Ethiopian Airline yaua abiria 149 na wafanyakazi 8 Ethiopian Airline yaua abiria 149 na wafanyakazi 8 Reviewed by Zero Degree on 3/10/2019 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.