Loading...

Kagere atangazwa kuwa mchezaji bora Ligi Kuu


MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Meddie Kagere amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.

Kagere raia wa Rwanda ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salim Aiyee wa Mwadui na Salum Kimenya wa Prisons alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa mwezi huo wa Februari, Simba ilicheza michezo mitano na kushinda yote, ambapo Kagere alitoa mchango mkubwa kwa timu yake kupata pointi 15 akifunga mabao matano na Simba kupanda kwa nafasi moja kutoka ya nne iliyokuwepo mwezi Januari katika msimamo wa ligi inayoshirikisha timu 20.

Kwa upande wa Aiyee alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timu ya Mwadui kwa mwezi huo, ambapo timu yake ilicheza michezo mitano ikishinda mitatu na kupoteza miwili ikipata pointi tisa na kupanda katika msimamo kutoka nafasi ya 15 hadi ya tisa na mshambuliaji huyo akipachika wavuni mabao manne.

Mafanikio ya Prisons kwa mwezi Februari ikishinda michezo yote mitano iliyocheza na kupata pointi 15 ikipanda kutoka nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi hadi ya 14 yamemuingiza katika fainali ya tuzo hizo mchezaji Salum Kimenya kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha na kuisaidia timu yake kupata mafanikio hayo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu.
Kagere atangazwa kuwa mchezaji bora Ligi Kuu Kagere atangazwa kuwa mchezaji bora Ligi Kuu Reviewed by Zero Degree on 3/06/2019 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.