Loading...

Nimetafakari na sasa nimeamua kurudi nyumbani - Lowassa


Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA Edward Lowassa amefunguka WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Edward Lowassa ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuanzia leo Machi 1,2019.

Akizungumza leo katika Ofisi za ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam,Lowassa hakuwa na maneno mengi ya kueleza zaidi ya kuwaambia Watanzania kuwa ameamua kurudi nyumbani (CCM).

"Nimetafakari na sasa nimeamua kurudi nyumbani CCM ambako sehemu kubwa ya maisha yangu nimekuwa huko,"amesema Lowassa huku mamia ya wananchi wakiwamo wanachama na wapenzi wa CCM walikuwa wanamshangilia.

Wakati Lowassa anatangaza kurejea CCM alikuwa amesikindikizwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga ambaye pia aliwahi kuwa Mtunza wa fedha wa CCM Rostam Aziz.

Lowassa aliondoka CCM na kwenda upinzani katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Aliondoka CCM na kwenda upinzani baada ya jina lake kukatwa katika kugombea urais kupitia Chama hicho.

Hivyo alipata ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chadema waliokuwa wameunganisha nguvu na vyama vingine vinne vya siasa vilivyokuwa vimeunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Akiwa upinzani Lowassa aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema lakini kuna kipindi aliamua kwenda Ikulu kufanya mazungumzo na Rais Dk.Magufuli ambapo baada ya kukutana na Rais alisema amevutiwa na utendaji kazi wake na anampongeza.
Nimetafakari na sasa nimeamua kurudi nyumbani - Lowassa Nimetafakari na sasa nimeamua kurudi nyumbani - Lowassa Reviewed by Zero Degree on 3/02/2019 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.