Loading...

Ramani ya uwanja mpya utakaojengwa Dodoma yatinga kwa JPM


Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na wataalamu wa ujenzi wa uwanja wa soka unaotarajiwa kujengwa Jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na wataalam wa ujenzi wa uwanja kutoka Morocco na Tanzania pamoja na Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Abdelillah Benry, yameshuhudiwa Rais Magufuli akioneshwa ramani ya uwanja huo.

Baada ya mazungumzo na Rais Magufuli, balozi huyo wa Morocco amesema kuwa, " tumekuwa na mazungumzo kuhusiana na mipango ya maendeleo kati ya Morocco na Tanzania. Kwa sasa tuna miradi mikubwa miwili tunaisimamia, ambayo ni ujenzi wa msikiti pamoja na uzinduaji wa ujenzi wa Uwanja wa Soka", amesema balozi Benry.

Ramani ya Uwanja mpya wa soka utakaojengwa Jijini Dodoma

Uwanja huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco, Mohamed VI katika eneo la Nara Jijini Dodoma, barabara ya kuelekea Singida ambapo jumla ya hekari 143 zimetengwa. Unatarajia kugharimu sh bilioni 56 na ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji zaidi ya 60,000 watakaoketi kwenye siti.

Sambamba na ujenzi wa uwanja wa soka, pia kitajengwa kituo cha michezo ambacho kitakuwa kilomita 3 kutoka kwenye uwanja huo.
Ramani ya uwanja mpya utakaojengwa Dodoma yatinga kwa JPM Ramani ya uwanja mpya utakaojengwa Dodoma yatinga kwa JPM Reviewed by Zero Degree on 3/13/2019 04:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.