Loading...

Serengeti Boys yachapa mtu 3-2 Uturuki


Kikosi cha Serengeti Boys kimeamka na kuitwanga Australia kwa mabao 3-2 katika mechi ya michuano ya Uefa Assist inayoendelea mjini Antalya.

Serengeti Boys ilianza mechi hiyo kwa kusua baada ya kuwaruhusu Australia kutangulia kabla ya kusawazisha katika dakika ya Edmund John katika dakika ya 16.

Kabla ya kwenda mapumziko, Australia waliandika bao la pili na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili, Serengeti Boys walianza kwa kushambulia kama mbogo hadi walipofanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 81, mfungaji akiwa ni Alphonce John.

Baada ya bao hilo, Serengeti Boys waliongeza mashambulizi na kuonyesha kuwazidi nguvu Australia kabla ya kupata bao la tatu katika dakika ya 89 mfungaji akiwa ni Kelvin John.

Katika mechi ya kwanza ya michuano ya Uefa Assist, Serengeti Boys ilipoteza kwa bao 1-0.

Imebaki mechi moja ambayo itachezwa keshokutwa Ijumaa na kesho asubuhi, Serengeti Boys watafanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuwavaa wenyeji Uturuki ambao pia wameshinda mechi moja na kupoteza moja.
Serengeti Boys yachapa mtu 3-2 Uturuki Serengeti Boys yachapa mtu 3-2 Uturuki Reviewed by Zero Degree on 3/06/2019 05:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.