Loading...

Balozi Kairuki asifu ripoti ya kazi za serikali ya China


Balozi wa Tanzania nchini China Bw Mbelwa Kairuki ameisifu ripoti ya kazi za serikali iliyotolewa na waziri mkuuwa China Bw Li Keqiang katika ufunguzi wa mkutano wa pili wa awamu ya 13 wa Bunge la Umma la China.

Balozi Kairuki ametaja baadhiya mambo muhimu kwenye ripoti hiyo, kuwa sera ya ajira kwanza ya China aliyotajaWaziri Mkuu Li kwenye ripoti yake inatilia maana ni maisha ya wananchi wake.

Amesema sera hiyo inatambua kuwa ajira ndiyo ni msingi wa utu wa raia wa China, na ajira ndio msingi wa kukua uchumi wa nchi Amesema China itazidi kusonga mbele kwa kuweka mkazo kwenye suala la ajira na kuhimiza maendeleo ya uchumi.

Balozi Kairuki pia amesema katika ripoti Waziri Mkuu ametaja baadhi ya ya changamoto zinazoikabili China, na mambo ambayo China itayaboresha ili kuvutia uwekezaji kutoka nchi za nje na kupanua soko.

Waziri mkuu wa ChinaLi Keqiang ameelezea kwamba China itaondoa vikwazo vilivyopo vinavyoathiri uwekezaji, na pia itapunguza ushuru na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Balozi Kairuki amesemakuna mambo yaliyomo kwenye hotuba hiyoambayo wamejifunza na watayapeleka kwenye nchi zao, ili kubadilishana uzoefu na kuiga mambo yanayoendana na mahitaji ya nchi husika.

Chanzo: Habari Leo
Balozi Kairuki asifu ripoti ya kazi za serikali ya China Balozi Kairuki asifu ripoti ya kazi za serikali ya China Reviewed by Zero Degree on 3/06/2019 05:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.