Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 2, 2019



Harry Kane amewaacha wachezaji wa Tottenham katika hofu kubwa kuwa anaweza kufikiria kuondoka endapo klabu hiyo itashindwa kubeba taji lolote tena msimu huu. (Telegraph)

Manchester United wako tayari kutumia kiasi cha pauni milioni 154 kusajili nyota wawili wa Benfica Ruben Dias na Joao Felix. (Daily Star)

Real Madrid wameshindwa kumvumilia Gareth Bale na wanapanga kumuuza kwenye majira ya joto.

Mmiliki wa klabu ya Bolton, Ken Anderson ameomba msamaha kwa kushindwa kuwalipa wachezaji wake mshara na kueleza kuwa kuna mpango wa kuiuza klabu hiyo hivi karibuni. (Sun)

Huddersfield wamemwondoa Jason Puncheon kikosini baada ya winga huyo kutofautiana na meneja Jan Siewert.

Maro Itoje anaweza kurejea kwenye kikosi cha timu ya taifa ya dhidi ya Italia katika dimba la Twickenham Jumamosi ijayo, baada ya kupitia kipindi cha mazoezi makali. (Daily Mail)

Brendan Rodgers anasistiza kuwa aliaacha kuwaambia wachezaji wa Celtic kuhusu mpango wake wa kujiunga na Leicester City kwa kuwa alihofia kuvunja morali yao. (Record)

Juventus inaripotiwa kuwa na mpango wa kujiunga kwenye mbio za kuwania saini ya aliyekuwa kocha wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane, ambaye hivi karibuni amekuwa akihusishwa na klabu ya Chelsea.

Kulingana na Ian Holloway, Fulham wamefanya kosa kubwa sana kumfukuza kazi Claudio Ranieri baada ya siku 106 akiwa kama meneja wa klabu hiyo.

Jose Mourinho anaweza kurejea katika moja ya klabu aliyoinoa zamani kwenye majira ya joto. (talkSport)

Jorginho

Jorginho anaamini bado ana uwezo wa kubadili fikra za mashabiki wa klabu ya Chelsea.

Nyota wa Manchester United Antonio Valencia anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto.

Kwa mujibu wa taarifa ya Unai Emery, Arsenal inaweza kumaliza ligi kuu ya Uingereza katika nafasi ya juu zaidi kuliko Tottenham. (ESPN)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 2, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 2, 2019 Reviewed by Zero Degree on 3/02/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.