Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Machi 11, 2019


Manchester City inamfuatilia kiungo wa kati wa Lyon, Tanguy Ndombele kwa lengo la kumnunua kiungo huyo wa miaka 22 -msumu huu wa joto.

Ndombele, pia anafutiliwa na Tottenham, Manchester United na Juventus

Tottenham na Arsenal huenda wakashindania saini ya kiungo wa kati wa klabu ya Villarreal, Pablo Fornals, 23.

Taarifa zinadai kuwa Gunners huenda wakamuuza Mesut Ozil kabla ya kuchukua hatua hiyo. 

Kilmarnock imetoa ofa ya awali kabla ya kuingia mkataba na kiungo wao wa kati wa zamani, Craig Bryson, 32, wa Derby ambaye mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu. (Express)

Pep Guardiola, ambaye hivi karibuni alihusishwa na Juventus, amewaambia marafiki zake kuwa yuko tayari kusalia Manchester City kwa miaka minne ijayo.

West Brom itafanya mazungumzo zaidi na meneja wa zamani wa Fulham, Slavisa Jokanovic siku ya Jumatatu wanapoendelea na kampeini ya kumsaka kocha mpya baada ya Darren Moore kufutwa kazi. (Telegraph)

Guardiola ametilia shaka hatima ya kiungo wa kati, Ilkay Gundogan katika klabu ya Manchester City baada kufichua kuwa mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 28 huenda usiongezwe. (Mirror)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20, ambaye amehusishwa na Real Madrid, amepuuzilia mbali tetesi kwamba huenda akaondoka Paris St-Germain msimu ujao. (Squawka)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemkosoa Eden Hazard kwa kutocheza vizuri licha ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Wolves.

Giovani Lo Celso

Tottenham huenda ikamnunua kiungo wa kimataifa wa Argentina, Giovani Lo Celso, ambaye amefunga mabao 12 akiwa Real Betis kwa mkopo kutoka Paris St-Germain msimu huu, ikiwa Christian Eriksen, 27, ataondoka klabu hiyo kujiunga na a Real Madrid. (Talksport)

Hatahivyo Betis inaonekana kunda imefanya uamuzi wa kumsaini Lo Celso -ambaye pia analengwa na Real Madrid - kwa mkataba wa kudumu wa euro milioni 21.5 msimu wa joto. (Marca)

Meneja wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekanusha madai kuwa kipa wao David de Gea aliathiriwa na mzozo unaoendelea kuhusiana na mkataba wake wakati wa mechi yao dhidi ya Arsenal ambapo walifungwa mabao 2-0. (Evening Standard)

Celtic inapania kumsaini mlinzi wa Chelsea, Tomas Kalas, 25, amabye anachezea Bristol City kwa mkopo. (Daily Record)

Chelsea imemweka meneja wa Wolves Nuno Espirito Santo katika orodha yao uhamisho wa mameneja. (Star)

Mlizi nguli Sergio Ramos, 32, ana mpango wa kuondoka Real Madrid msimu huu ikiwa klabu hiyo itamuajiri meneja wao wa zamani Jose Mourinho. (Daily Mail)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Machi 11, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Machi 11, 2019 Reviewed by Zero Degree on 3/11/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.