Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 9, 2019


Real Madrid wanajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 300 kumnasa Neymar ili kujaza pengo la Cristiano Ronaldo.

Nyota wa klabu ya Real Madrid Isco amekasirishwa na meneja wa klabu hiyo Santiago Solari na amemwambia wakala wake afanye mawasiliano na klabu ya Manchester City kuhusu uhamisho wake.

Adhabu ya Chelsea imeongeza uwezekano wa Eden Hazard kuondoka katika klabu hiyo bure wakati mkataba wake utakapoisha mwaka 2020. (Sun)

Klabu ya Tottenham imakunusha taarrifa zinazodai kuwa uwanja wao mpya utaitwa 'The Nike Stadium'.

Ryan Giggs amepanga kufanya mazoezi na kikosi chake cha Wales katika uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington kuelekea mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Trinidad & Tobago.

Bournemouth wanatarajia kumkosa beki wao Steve Cook kwa muda wa kaibu wiki sita baada ya jeraha lake la kiunoni kupata maambukizi mapya.

Wolves inakazania kukamilisha usajili wa mshambuliaji chipukizi wa klabu ya Birmingham City, Ramello Mitchell. (Daily Mail)

Pep Guardiola

Pep Guardiola amekubali kuchukua majukumu ya kukinoa kikosi cha Juventus mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa ripoti za nchini Italia. (Express)

Arsenal wanamatumaini ya kumshawishi Monchi awe mkurugenzi wao wa michezo, lakini Mhispania huyo anasema kuwa bado hajaamua kama atachukua jukumu hilo au la. (Guardian)

Gareth Southgate ana matumaini ya kuona kiwango cha nyota wa klabu ya Bournemouth Callum Wilson dhidi ya Huddersfield kama mshambuliaji yuko tayari kurejea dimbani baada ya kuumia goti. (Telegraph)

Mauricio Pochettino amesema kuwa amehisi kuheshimiwa kusikia klabu ya Real Madrid inahitaji huduma yake na kudai kuwa anaweza kufikiria kurejea kufanya kazi Hispania.

Watford wanaweza kuitaka Manchester City katika meza ya usuluhishi baada ya klabu hiyo kupoteza nafasi ya kumuuza Jadon Sancho mwaka 2015. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 9, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 9, 2019 Reviewed by Zero Degree on 3/09/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.