Kwanini Pochettino anashauriwa kumpiga benchi Harry Kane kwenye fainali ya UEFA
Tottenham Hotspur walifuzu hatua ya nusu fainali michuano hiyo dhidi ya Ajax bila mshambuliaji huyo. Kane alijiunga na mazoezi ya timu yake wiki iliyopita na kudai kwamba anaweza kumudu mikiki ya fainali hiyo dhidi ya Liverpool ndani ya wiki moja.
Hata hivyo, Chris Sutton amemshauri meneja wa Spurs kutomjumuisha Kane kwenye kikosi chake cha kwanza. Alisema, “Harry Kane hatakiwi kuanza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa. Ni hatari sana kwa Tottenham katika mchezo huo muhimu na meneja Mauricio Pochettino lazima afanye uamuzi mgumu. Hata kama Kane anasema yuko vizuri, lazima kutakuwa na shaka juu ya afya yake.
“Mara ya mwisho mshambuliaji huyo kuonekana dimbani na Spurs ilikuwa ni dhidi ya Manchester City April 9 na Jumatatu akaibuka na kusema kuwa amerejea mazoezini tangu mwisho wa wiki iliyopita.
“Anaweza kufanya mazoezi pamoja na timu yake lakini hiyo ni tofauti na mechi ya kweli kweli. Liverpool na Tottenham haitakuwa mchezo rahisi kwani kila mmoja atakuwa makini na kunaweza kusiwe na nafasi kwa wasafiri wa kutalii mjini Madrid.
“Naelewa ni kwanini Kane anajiweka mbele na kumweleza meneja wake kuwa anataka kucheza. Kwani ni nahodha gani asingeweza kufanya hivyo? Lakini Pochettino atatakiwa kujiuliza: Kama kumjumuisha Kane kwenye kikosi cha kwanza inaweza kuwa na faida kwa timu au la? Sidhani kama itakuwa sahihi. Nani atakayeachwa ili kutoa nafasi kwa Kane? Lucas Moura, ambaye 'hat-trick' dhidi ya Ajax kwenye nusu fainali iliwafikisha hadi hatua hiyo ya kukutana na Liverpool?
“Son Heung-min, mshambuliaji matata, ambaye amekuwa sehemu muhimu kwenye kikosi cha Spurs msimu huu? Hakuna hata mmoja kati ya hao unaweza kufikilia kumwacha. Kama Kane angekuwa amerejea mazoezini kwa muda, na kushiriki katika michezo kadhaa, hivyo, bila shaka, ungeweza kumjumuisha kikosini.
“Lakini hali iko tofauti, hivyo lazima atiliwe shaka. Kane anaweza kugeuka na kuwa sila hatari akitokea benchi. Pochettino ana wakati mgumu kufanya uamuzi na lazima awe makini kuhusiana na hilo.”
Hata hivyo, Chris Sutton amemshauri meneja wa Spurs kutomjumuisha Kane kwenye kikosi chake cha kwanza. Alisema, “Harry Kane hatakiwi kuanza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa. Ni hatari sana kwa Tottenham katika mchezo huo muhimu na meneja Mauricio Pochettino lazima afanye uamuzi mgumu. Hata kama Kane anasema yuko vizuri, lazima kutakuwa na shaka juu ya afya yake.
“Mara ya mwisho mshambuliaji huyo kuonekana dimbani na Spurs ilikuwa ni dhidi ya Manchester City April 9 na Jumatatu akaibuka na kusema kuwa amerejea mazoezini tangu mwisho wa wiki iliyopita.
| Harry Kane |
“Naelewa ni kwanini Kane anajiweka mbele na kumweleza meneja wake kuwa anataka kucheza. Kwani ni nahodha gani asingeweza kufanya hivyo? Lakini Pochettino atatakiwa kujiuliza: Kama kumjumuisha Kane kwenye kikosi cha kwanza inaweza kuwa na faida kwa timu au la? Sidhani kama itakuwa sahihi. Nani atakayeachwa ili kutoa nafasi kwa Kane? Lucas Moura, ambaye 'hat-trick' dhidi ya Ajax kwenye nusu fainali iliwafikisha hadi hatua hiyo ya kukutana na Liverpool?
“Son Heung-min, mshambuliaji matata, ambaye amekuwa sehemu muhimu kwenye kikosi cha Spurs msimu huu? Hakuna hata mmoja kati ya hao unaweza kufikilia kumwacha. Kama Kane angekuwa amerejea mazoezini kwa muda, na kushiriki katika michezo kadhaa, hivyo, bila shaka, ungeweza kumjumuisha kikosini.
“Lakini hali iko tofauti, hivyo lazima atiliwe shaka. Kane anaweza kugeuka na kuwa sila hatari akitokea benchi. Pochettino ana wakati mgumu kufanya uamuzi na lazima awe makini kuhusiana na hilo.”
Kwanini Pochettino anashauriwa kumpiga benchi Harry Kane kwenye fainali ya UEFA
Reviewed by Zero Degree
on
5/28/2019 02:35:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
5/28/2019 02:35:00 PM
Rating: