Loading...

Mashabiki watamani Beckham arejee Old Trafford


David Beckham ametakiwa kurejea uwanjani katika kikosi cha Manchester United.

Idadi kubwa ya mashabiki wamemtaja Beckham kuwa ni mchezaji wa aina yake katika medani ya soka Uingereza. 

Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza, alikuwa nyota wa mchezo wa kirafiki wa kumbukumbu ya miaka 20 ya mechi ya fainali baina ya Man United dhidi ya Bayern Munich. Man United ilishinda mabao 2-1. Katika mechi ya juzi usiku iliyowakutanisha nyota wa zamani wa timu hizo kwenye Uwanja wa Old Trafford, Man United ilishinda mabao 5-0.

Moja ya mambo ya kuvutia yaliyoonyeshwa na nguli huyo ni kitendo chake cha kupiga mipira ya krosi iliyokuwa maarufu enzi zake.





Licha ya kuwa na umri wa miaka 44, Beckham alicheza kwa kiwango bora na kuwa kivutio kwa mashabiki.

Baada ya kumaliza vibaya katika Ligi Kuu England ikishika nafasi ya sita katika msimamo, mashabiki wa klabu hiyo waliandika katika mitandao kuwa nyota huyo anastahili kurejea Old Trafford.
Mashabiki watamani Beckham arejee Old Trafford Mashabiki watamani Beckham arejee Old Trafford Reviewed by Zero Degree on 5/28/2019 06:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.