Loading...

Tembo auwa wawili ajeruhi watano


Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay (CCM) ameomba mwongozo bungeni akitaka Serikali impe majibu kuhusiana na tembo ambao wameua watu wawili na kujeruhi watano katika Jimbo lake.

Akiomba mwongozo leo Mei 28 bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Massay amemesema kwamba Tembo wameua watu wawili na wanaendelea kufanya uharibifu katika Jimbo lake.

“Mhehimiwa Mwenyekiti naomba mwongozo jambo hili limekuwa hatari na tembo wanaendelea kufanya uharibifu na watu watano wapo Hospital wakiwa wamejeruhiwa.

“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba Serikali inisaidie kule kwa sababu tembo ni hatari wameendelea kuua watu wengi Jimboni,”amesema

Akijibu, Mwenyekiti wa Bunge,Najma Giga amesema “Naamini Serikali wameshalisikia, kuhusiana na vitendo vinavyohusiana na jambo hilo naamini kwamba watalifuatilia.

Chanzo: Mtanzania
Tembo auwa wawili ajeruhi watano Tembo auwa wawili ajeruhi watano Reviewed by Zero Degree on 5/28/2019 06:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.