Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Mei 29, 2019


Atletico Madrid wamemchagua mshambuliaji wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Uruguay Edinson Cavani, 32, kama mbadala wa mshambuliaji wao Diego Costa, 30. (Cadena Ser)

Mshambuliaji wa Manchester United Mbelgiji Romelo Lukaku, 26, yupo tayari kukatwa mshahara ili ahamie klabu ya Inter Milan hivi karibuni. (Gazzetta dello Sport)

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer ameipa klabu yake mpaka mwakani kuuza wachezaji wote asiowataka ikiwa kama sehemu ya miango yake ya kuijenga upya klabu hiyo. (MEN)

Barcelona wameamua kuendelea na kocha Ernesto Valverde kwa msimu ujao japo kulikuwa na ripoti kuwa kocha huyo alikuwa afutwe kazi. (Marca)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema ana matumaini ya kumsajili Eden Hazard, 28, katika majira haya ya joto. (Onda Cero)

Newcastle United wamefanya mawasiliano na klabu ya Benfica wakiwa na nia ya kumsajili kipa wao raia wa Ugiriki Odysseas Vlachodimos, 25, na inaaminika Benfica wanataka kitita cha pauni milioni 13. (O Jogo)

Barcelona pia inasemekana wapo tayari kumtoa kiungo Philippe Coutinho, 26, ama mshambuliaji Ousmane Dembele, 22, kwenda Paris St-Germain kama sehemu ya makubaliano ya kumpata mshambuliaji Neymar, 27. (Record)

Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte amesaini mkataba mpya wa kuinoa klabu ya Inter Milan mpaka mwaka 2022. (Tuttomercatoweb)

Streka wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic yaonekana hana nia ya kuendelea kusakata kabumbu kwenye klabu hiyo baada ya kuhamisha viurago vyake kwenye kabati lake la timu kabla ya michuano ya Ulaya ya wachezaji wa chini ya miaka 21. (Bild)

Kocha wa klabu ya Arsenal Unai Emery anataka kumsajili beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Ubelgiji Thomas Meunier, 27, kutoka katika klabu ya Paris St-Germain. (France Football)

Jerome Roussillon, 26

Barcelona wanataka kumsajili beki wa kushoto wa klabu ya Wolfsburg raia wa Ufaransa Jerome Roussillon, 26, baada ya kuwakuna wachunguzi wa klabu hiyo waliokuwa wakimuangalia kipa wa timu hiyo Koen Casteels, 26. (Mundo Deportivo)

Timu iliyopanda daraja Ligi ya Primia Aston Villa itaanza maandalizi ya michuano hiyo kwa kutuma nia ya kumsajili mshambuliaji wa Nottingham Forest Joe Lolley, mwenye thamani ya pauni milioni 10. (Daily Mail)

Beki wa kulia wa klabu ya Tottenham na England Kieran Trippier, 28, hatasainiwa tena na klabu ya Napoli baada ya timu hiyo kuelekeza nguvu zake kwa wachezaji kinda. (Sun)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Mei 29, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Mei 29, 2019 Reviewed by Zero Degree on 5/29/2019 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.