Harmonise afunga ndoa kwa siri
Msanii Rajab Abdul Kahali kwa jina maarufu Harmonize amefunga ndoa na mchumba wake ambaye ni raia wa Italia, Sarah Michelotti siku chache baada ya mwanamuziki huyo kujiondoa rasmi katika kundi la Wasafi Classic Baby WCB ambalo linaongozwa na msanii kinara nchini Tanzania, Diamond Platnums.
Mwanamuziki huyo anayependa kujiita konde boy akimaanisha kuwakilisha wamakonde kutoka kusini mwa Tanzania alimchumbia Sarah miezi michache iliyopita na hakuwahi kutangaza siku rasmi ya harusi yake.
Harusi hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya siri ilifanyika jumamosi ya tarehe 7, Septemba 2019 jijini Dar es salaam na kuhudhuria na wageni 100 tu.
Si jambo la kawaida kwa harusi nchini Tanzania kuhudhuriwa na watu wachache kiasi hicho hata kwa watu ambao si maarufu.
Gazeti la The Citizen nchini Tanzania limeandika kuwa hakuna msanii hata mmoja kutoka kundi lake la zamani la Wasafi aliyeudhuria tafrija hiyo ya mwana muziki huyo.
Pongezi nyingi kwake zimetoka kwa mashabiki na wadau wa tasnia kwa hatua ambayo amepiga na kutajwa kuwa mfano wa kuigwa:

Hongera sana Sarah kupata Dume. Mungu abarike Ndoa ya Sarah na Rajabu .ameen. pic.twitter.com/Kh1ydiVAZv— Mustafa Hassanali (@mustafahasanali) September 7, 2019
Wakati harusi hiyo ikiwashangaza wengi katika mitandao ya kijamii, wengine wakidai kuwa labda ndoa ndio ilikuwa sababu kuu ya mwanamuziki huyo kuacha kuimba na Diamond.
Oiii Ankal @harmonize_tz HONGERA SANA KWA MAISHA HAYA MAPYA UNAYOKWENDA KUYAANZA 💪— DJ CHOKA 🇹🇿 (@ChokaDJ) September 8, 2019
MUNGU IBARIKI NDOA HII NA IKADUMU MIAKA MINGI NA HERI DUNIANI 🙏#DJChoka pic.twitter.com/8qMHPNXKtW
Harmonize kwa sasa anasifika kwa wimbo unaompongeza rais Magufuli katika utendaji wake wa kulijenga taifa unaoitwa 'magufuli'.
Harmonise afunga ndoa kwa siri
Reviewed by Zero Degree
on
9/09/2019 10:50:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
9/09/2019 10:50:00 AM
Rating: