Loading...

Kiungo Mtibwa Sugar awaondoa hofu mashabiki


KIUNGO wa Mtibwa Sugar, Awadhi Juma, amesema licha ya kuanza vibaya Ligi Kuu Tanzania Bara, timu yao itarudi katika mstari, kwani mapema mno kukata tamaa.

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Bingwa, Awadhi alisema anauhakika wa kufanya vizuri mchezo ujao.

Awadhi alisema pamja na kupoteza michezo mitatu huku wakitoka sare moja, bado wana matumani ya kupata matokeo bora.

Alisema watahakikisha wanajipanga upya na kurekebisha kasoro yaliyojitokeza ili waweze kumaliza hasira zao kwa timu ambayo watakutana nayo.

“Tumeanza vibaya, huu ni mpira na sio kila mwaka utafanya kama ilivyoanza mwaka uliopita, mambo yanabadilika lakini hii haimaanishi kuwa tutamaliza vibaya.

Tumepoteza pointi tatu katika uwanja wa nyumbani,naamini kuanzia mchezo ujao kikosi kitakuwa kikifanya vizuri,” alisema Awadhi

Mtibwa Sugar ilianza ligi hiyo kwa kufungwa na Lipuli mabao 3-1, kasha ilifungwa na Simba mabao 2-1 kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania na baadaye kufungwa na Tanzania Prisons mabao 3-1.
Kiungo Mtibwa Sugar awaondoa hofu mashabiki Kiungo Mtibwa Sugar awaondoa hofu mashabiki Reviewed by Zero Degree on 9/27/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.