Loading...

Ofisa wa CRDB kortini kwa madai ya kumuibia mteja


Ofisa wa Benki ya CRDB, Andrew Babu na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka nane likiwemo la kuiba na kutakatisha fedha kiasi cha Sh106 milioni.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuiba fedha kwa kutumia kadi ya Viza Gold mali ya Charles Kihamia.

Mbali na Babu, washitakiwa wengine ni William Sige, Justina Boniphas na Ally Tatupa ambao wote wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 101/2019.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amewasomea mashtaka yao jana Alhamisi Septemba 26, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Agustina Mbando.

Simon amedai washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Oktoba 7, 2018 hadi Aprili 29, 2019 katika Benki ya CRDB iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika tarehe hizo, washtakiwa hao waliiba Sh106.26 milioni mali ya Charles Kihamia.
Ofisa wa CRDB kortini kwa madai ya kumuibia mteja Ofisa wa CRDB kortini kwa madai ya kumuibia mteja Reviewed by Zero Degree on 9/28/2019 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.