Loading...

Rais Ramaphosa amteua Pro. Ndulu kuwa mshauri wake


Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa jana Ijumaa Septemba 27, 2019 amemteua aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu kuwa mshauri wake wa masuala ya uchumi.

Profesa Nduru anaungana na wenzake 17 wanaounda baraza la wataalam wa uchumi linalomshauri Rais Ramaphosa.

Watu hao kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini ni wabobezi katika uchumi wa kimataifa, uchumi mkubwa katika masuala ya kodi na fedha.

Taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya rais Ramaphosa inaeleza kuwa Profesa Ndulu amebobea katika kuanzisha na kuendeleza tafiti, mafunzo na mikutano ya tafiti za uchumi Afrika.

Inaeleza kuwa baraza hilo litaanza kazi Oktoba Mosi, 2019 na kuendeshwa na Rais Ramaphosa katika kipindi cha miaka mitatu.

Ndulu ameongoza BoT kuanzia mwaka 2008 hadi 2018 baada ya Rais John Magufuli kumteua Profesa Florens Luoga kushika nafasi hiyo.
Rais Ramaphosa amteua Pro. Ndulu kuwa mshauri wake Rais Ramaphosa amteua Pro. Ndulu kuwa mshauri wake Reviewed by Zero Degree on 9/28/2019 07:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.