Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Septemba 27, 2019


Manchester United wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele, mwenye umri wa miaka 23, ambapo wametuma ujumbe wake kumfuatilia mchezaji huyo katika mechi tatu.

Mkuu wa zamani wa Chelsea na Manchester United Peter Kenyon ameanza mchakato mpya wa kuinunua Newcastle kwa ushirikiano na mkewe kwa kumlipa mmiliki wake Mike Ashley pauni milioni 125 kwanza. (Mail)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, atachukua hatua mpya ya kuondoka mwezi Januari.

Manchester United awako tayari kulipa pauni milioni 32 ili kutimiza kigezo kinachotakiwa kwa ajili ya meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino.

Mkataba wa ununuzi huo unadai kuwa meneja wa Newcastle manager Steve Bruce amepata mafanikio "yasiyoweza kulinganishwa Ulaya ".

Crystal Palace wanaangalia uwezekani wa kumnunua mlinzi wa safu ya kati wa Shakhtar Donetsk Taras Stepanenko, mwenye umri wa miaka 30, baada ya kukosa fursa ya usaini mkataba na mchezaji huyo wa kimataifa wa ukraine kwa pauni milioni 8 msimu huu. (Sun)

Mshambuliaji wa klabu ya Paris St-Germain Neymar, mwenye umri wa miaka 27, amewasili nchini Uhispania kwa ajili ya kesi dhidi ya klabu yake ya zamani Barcelona juu ya kusaini mkataba usio na malipo kuhusu faida. (Mundo Deportivo)

Barcelona na Atletico Madrid watakata rufaa juu ya uamuzi wa kuitoza faini Barca euro 300 (£265) kutokana na namna walivyowasiliana na mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann alipokuwa Atletico. (Marca)

Nahodha wa zamani wa England David Beckham amepanga kuwa wakala wa soka - huku mshambuliaji wa United Mason Greenwood, mwenye umri wa miaka 17, akiwa na uwezekano wa kuwa mteja. (Mirror)

Klabu ya Fulham inataka fidia ya pauni milioni 7 kutoka Liverpool baada ya kiungo wa kati Harvey Elliott mwenye umri wa miaka 16 kujiunga na Reds msimu huu. (Times)

Wachezaji wa Arsenal walipiga kura kuamua ni nani atakayekuwa nahodha wa kikosi hicho huku meneja Unai Emery akiangalia mkakati wa kujenga upya uongozi wake unaowahusisha watu watano katika timu . (Telegraph)

Tammy Abraham, 21

Mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, mwenye umri wa miaka 21, "hakufurahia " kiwango ambacho FIFA ilimpa cha mchezaji nambari 20 baada ya kupokea "zawadi ya kipekee " katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea. (Star)

Mshambuliaji wa Denmark Kasper Dolberg, mwenye umri wa miaka 21, aliibiwa saa ya pauni 62,000 katika kiwanja cha mazoezi cha Nice mwezi huu na mchezaji mwenza Lamine Diaby-Fadiga mwenye umri wa miaka 18-anashukiwa kuichukua . (L'Equipe)

Waandalizi wa Kombe la dunia 2022 nchini Qatar wamekamilisha mkataba ambao utawezesha kupunguzwa kwa bei ya pombe wakati wa mashindano ya kombe hilo. (Guardian)

Newcastle wamekuwa wakimchunguza kwa karibu mlinzi wa Rochdale Luke Matheson mwenye umri wa miaka 16, aliyefunga bao dhidi ya Manchester United Jumatano , tangu alipojiunga na timu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka jana. (Chronicle)

Huddersfield wanatumai kusaini mkataba na mlinzi Danny Simpson mwenye umri wa miaka 32-ambaye amekuwa huru tangu alipoondoka Leicester msimu huu . (Yorkshire Post)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Septemba 27, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Septemba 27, 2019 Reviewed by Zero Degree on 9/27/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.