Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Septemba 28, 2019


Pep Guardiola amekiri kuwa anafanya kazi kubwa kumfanya Gabriel Jesus awe na furaha katika klabu ya Manchester City kutokana na kukosa nafasi ya mara kwa mara uwanjani.

Wamiliki wa klabu ya Manchester City wanatarajiwa kukamilisha dili la kuinunua klabu ya ligi kuu ya India, Mumbai City kuelekea mwanzo wa msimu mpya unataotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Mirror)

Wachezaji wa Spurs wamekasilishwa na madai yaliyotolewa na Mauricio Pochettino baada ya klabu hiyo kufungwa kwenye mchezo wa Carabao Cup dhidi ya Colchester.

Neymar alipuuzia ratiba inayomsubiri kutokea mahakamani ili afurahie usiku pamoja na waliokua wachezaji wenzake wa Barcelona.

Ole Gunnar Solskjaer ameteua skauti wake binafsi afanye kazi ya kumtafutia wachezaji wa kusajili kwa lengo la kuirejesha United kwenye ngazi za juu za ushindani.

Aliyekuwa beki wa zamani wa klabu ya Chelsea, John Terry amenunua mbwa wa wa pauni 15,000 awe mlinzi wa kulinda mji wake. (Sun)


Harry Wilson ameeleza kuwa meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp anafuatilia maendeleo yake akiwa katika klabu ya Bournemouth kwa mkopo.

Meneja wa klabu ya Manchester City Pep Guadiola ameeleza kuwa klabu yake haina mpango wa kusajili wachezaji wapya mwezi Januari.

Ross Barkley


Kiungo wa klabu ya Chelsea, Ross Barkley anadai kuwa meneja wa klabu hiyo Frank Lampard anawapa viungo kipaumbele cha kufunga mabao. (SkySports)

Peter Kenyon alifanya mazungumzo na Washirika wa MSD, kampuni ya uwekezaji ambayo inakaribia kuinunua klabu ya Sunderland, kabla ya kukamilisha taratibu za kumpelekea Mike Ashley ofa ya pauni milioni 300 kuinunua Newcastle.

Liverpool imefanya mazungumzo ya awali na James Milner kuhusu mkataba mpya baada Jurgen Klopp kueleza kuwa kiungo huyo ana umuhimu mkubwa sana katika kikosi chake.

Frank Lampard anadai kuwa Callum Hudson-Odoi anaweza kuwa mchezaji bora zaidi kama atajirejea upya na kuitazama asili yake - na kufuata mfano ulioonyeshwa na Raheem Sterling. (Daily Mail)

Inasemekana ofa mpya ya utengenezaji wa jezi iliyotolewa na kampuni ya Nike kwa klabu ya Liverpool ina thamani ya pauni milioni 30 kwa mwaka. 
(Times)

Steve Bruce amepa kubadili mfumo katika klabu ya Newcastle kumaliza masalia yaliyoacha na aliyekuwa meneja wa klabu hiyo, Rafael Benitez. (Gurdian)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Septemba 28, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Septemba 28, 2019 Reviewed by Zero Degree on 9/28/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.