Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Septemba 29, 2019


Barcelona wanatarajiwa kurejea kwenye mpango wao wa kutaka kumsajili nyota wa klabu ya Chelsea Willian kama mchezaji huru, huku mkataba wake na klabu hiyo ukitarajiwa kuisha mwaka 2020.

Mkufunzi wa David de Gea, Emilio Alvarez ameondoka katika klabu ya Manchester United.

Imeripotiwa kwamba Paul Pogba amedai kulipwa kiasi cha pauni milioni 30 kwa mwaka kutoka Manchester United, mara mbili ya kiasi anacholipwa kwa sasa.

Wakala wa Victor Lindelof ameeleza kwamba Barcelona ilitoa ofa kadhaa kutaka kumsajili raia huyo wa Sweden kwenye majira ya joto yaliyopita. (Mail)

Tottenham wamemfanya Gareth Southgate kuwa chaguo lao la kwanza kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino kama akiondoka.

Manchester United wameamua kuwa hawatateua mkurugenzi wa kandanda hivi karibuni - shukrani kwa mafanikio yao kwenye biashara ya usajili wa wachezaji wa majira ya joto.

Usajili wa wachezaji wapya katika klabu ya Manchester United katikati ya msimu unategemea kwa sehemu kubwa kiwango atakachoonyesha Mason Greenwood kama mchezaji wa kikosi cha kwanza. (Star)

Jose Mourinho anaripotiwa kuwa na hamu kubwa ya kurejea kuinoa klabu ya Real Madrid.

Derby County hawana mkakati wa kuwafuta kazi Mason Bennett na Tom Lawrence - licha ya kuidhalilisha klabu hiyo kwa kukutwa wakiendesha gari wakiwa wamelewa.

Kieran Tierney yuko tayari kucheza dhidi ya Manchester United - lakini Arsenal wanatarajiwa kuingia dimbani bila Hector Bellerin.

Ununuzi wa klabu ya Sunderland na Kampuni ya uwekezaji ya Marekani uko kaibu kukwama baada ya mmiliki wa klabu hiyo Stewart Donald kuonekana kuwa mgumu kukubali bei ya klabu.

Kwa mijibu wa ripoti, wafanyakazi wa klabu ya Manchester City 'walitaka' klabu hiyo ifungiwe kufanya usajili kumshinikiza Pep Guardiola kuchezesha wachezaji chipukizi. (Sun)

Pep Guardiola anaungwa mkono na wachezaji wake wa Manchester City baada ya kuwapuuzia mabosi wa klabu hiyo kuanzisha shauri juu ya tuhuma za ubaguzi kwa Bernardo Silva.

Hofu ya wamiliki wa klabu ya Liverpool kwamba Jurgen Klopp anaweza kuwa tayari uondoka Anfield ikiwa itatokea ofa yoyote kutoka Ujerumani.

Giovanni van ­Bronckhorst

Manchester City wanajiandaa na maisha bila Pep Guardiola baada ya kumpa kocha Mholanzi Giovanni van ­Bronckhorst kibali cha kufika katika maeneo yote ya klabu hiyo.

Wolves wanamfukuzia kiungo mchezeshaji wa klabu ya Real Madrid Martin Odegaard, ambaye msimu huu yuko Real Sociedad kwa mkopo. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Septemba 29, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Septemba 29, 2019 Reviewed by Zero Degree on 9/29/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.