Loading...

Asimamishwa kazi Tanesco kisa umeme kukatika jijini Dar


Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dk Medard Kalemani amemsimamisha kazi muongoza mifumo ya umeme wa kituo cha kupoza nishati hiyo cha Ubungo jijini Dar es Salaam, Samson Mwangalume.

Amechukua uamuzi huo leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 baada ya usiku wa kuamkia leo umeme kukatika huku chanzo kikielezwa kuwa ni uchafu wa vikombe katika njia za kusafirisha nishati hiyo.

Dk Kalemani pia ametoa onyo la mwisho kwa kaimu meneja mwandamizi wa usafirishaji wa umeme, Amos Kahiyula kuhakikisha haukatiki kutokana na uzembe.

Ametoa maagizo mara baada ya kutembelea kituo hicho na kutoridhishwa na maelezo ya Kahiyula aliyetoa sababu hizo baada ya kutakiwa na waziri huyo kueleza chanzo.

"Haiwezekani watu mkae muda mrefu bila kutazama hali ya vikombe hadi viwe vichafu kiasi cha kusababisha umeme kukatika, huu ni uzembe usiokubalika kwani serikali imeshawekeza vya kutosha kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika.”

" Nataka huyo Samson aliyekuwa mkuu wa zamu asimamishwe kazi kuanzia leo na maelezo yake niyapate leo ofisini kwangu kwani kama ni vikombe vipo kwa nini hamkuviweka,” amesema Dk Kalemani.
Asimamishwa kazi Tanesco kisa umeme kukatika jijini Dar Asimamishwa kazi Tanesco kisa umeme kukatika jijini Dar Reviewed by Zero Degree on 10/03/2019 06:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.