Loading...

JPM apongezwa kwa kukemea mimba kwa wanafunzi mashuleni


Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), kimempongeza Rais John Magufuli, kwa kuzungumzia kwa uwazi na kukemea hadharani suala la ongezeko la mimba kwa wanafunzi mkoani Rukwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Rose Ruben, ilisema chama hicho miongoni mwa malengo yake ni kupunguza mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia.

Bi. Rose alisema mimba za utotoni zinaitia hasara serikali inayotoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya elimu bure, shule za msingi na sekondari, na kwamba mimba hizo ndicho chanzo cha vifo vya uzazi na maradhi ikiwamo Ukimwi.

Rais Magufuli jana akiwa ziarani mkoani Rukwa, Alisema kwa takwimu alizopata kulikuwa na wanafunzi 229 waliopata mimba mkoani humo mwaka jana pekee.

SOMA ZAIDI TAARIFA HIYO:

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinampongeza Rais John Magufuli kwa kuzungumza kwa uwazi na kukemea suala la ongezeko la mimba kwa wanafunzi mkoani Rukwa.

Rais Magufuli ambaye yupo ziarani mkoani Rukwa amesema kwa takwimu alizonazo, kulikuwa na wanafunzi 229 waliopata mimba mkoani humo mwaka jana pekee.

“Ninawaomba ndugu zangu, ninawaomba sana, na ndugu zangu wasukuma acheni kuwaoza watoto wakiwa wadogo, tuwaache watoto wasome. Kwa sababu inawezekana tabia hizi hazikuwepo Rukwa, 229 kwa mwaka hawa ni wale waliojulikana, je wale wasiojulikana ni wangapi? Niwaombe ndugu zangu, wakina mama tuwakanye watoto wetu, wakina baba tuwakanye watoto wetu , ili wakaipate hii elimu wakawe wakombozi wa maisha ya baadaye,” amesema Rais Magufuli leo.

TAMWA ambayo miongoni mwa malengo yake ni kupunguza mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia, imefurahishwa na jinsi Rais Magufuli anavyoguswa na changamoto hii ya mimba za utotoni nchini na kuikemea hadharani.

Kama Rais Magufuli alivyosema, mimba hizi za utotoni zinaitia hasara serikali inayotoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya elimu bure, shule za msingi na sekondari. Lakini si hivyo tu, bali mimba hizi ndicho chanzo cha vifo vya uzazi na pia chanzo cha maradhi ikiwamo Ukimwi.

Taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa baadhi ya wanaohusika katika kuwapa mimba wanafunzi ni walimu, polisi na madereva bodaboda wasiofuata maadili. Wakati makundi hayo yanaaminiwa katika kuwapa ulinzi wanafunzi.

Kama Rais Magufuli alivyosisitiza, TAMWA inawasihi wazazi na walezi wawafundishe watoto kuepuka vitendo vya ngono na tunaziomba taasisi za dini kuwaelimisha watoto wa kike kujiepusha na vitendo vya ngono. Pia tunawaomba viongozi wa dini watoe mawaisha kuwakanya wanaume wanaolaghai wanafunzi.

Pia tunaomba viongozi wa dini watoe mawaidha ya kuwakanya wanaume wanaowalaghai wanafunzi.

TAMWA imekuwa ikipigania haki za watoto wa kike na wanawake kwa ujumla na tunasisitiza kuwa tutaendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kupambana na kupunguza mimba za utotoni nchini kwa kutoa elimu kuanzia ngazi za vijiji, kata hadi ngazi ya mkoa.
JPM apongezwa kwa kukemea mimba kwa wanafunzi mashuleni JPM apongezwa kwa kukemea mimba kwa wanafunzi mashuleni Reviewed by Zero Degree on 10/09/2019 07:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.