Loading...

Katoni 328 za pombe bandia zanaswa mkoani Geita

Meneja wa TRA mkoani Geita, Hamisi Ngoda

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Geita imekamata katoni 328 za pombe bandia aina ya kasi vodka na Wakawaka Gin zilizokuwa zinaandaliwa kusambazwa kinyemela sokoni bila kulipa kodi.

Pombe hiyo inadaiwa kukamatwa na maofisa wa mamlaka hiyo juzi baada ya kuwekwa mtego kwa wafanyabiashara wanaosambaza vinywaji vya aina mbalimbali mkoani hapa.

Meneja wa TRA mkoani Geita, Hamisi Ngoda, akizungumza na gazeti hili, alisema katoni 230 za pombe hizo zilikamatwa na maofisa wa mamlaka hiyo zikiwa kwenye gari moja aina ya Toyota lenye namba za usajili T396 DFC mali ya kampuni ya( KASI PLUS (T) LIMITED) inayotengeneza pombe hizo, na baada ya kukaguliwa lilikutwa likiwa limesheheni katoni 230 za pombe hiyo ambazo zilikuwa tayari kuuzwa kwa wafanyabiashara hao.

Meneja huyo alisema kuwa katoni 97 za pombe hizo zilikamatwa na maofisa wa mamlaka hiyo kwenye maduka ya wafanyabiashara wawili ambao ni wasambazaji wa vinywaji vya pombe za aina mbalimbali wa mkoani Geita, na kuwa a mzigo huo unatakiwa kulipa kodi ya zaidi ya Sh. milioni 7.

Aidha, Ngoda alisema mamlaka hiyo inalishikilia gari la kampuni hiyo na wafanyabiashara wawili ambao hapa msambazaji wa pombe hizo na dereva wa gari hilo, na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea kwenye kiwanda cha kampuni hiyo Kibaha.

Pia aliwaonya wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi ya serikali mkoani humo kuwa mamlaka hiyo imejipanga kuwadhibiti kikamilifu.
Katoni 328 za pombe bandia zanaswa mkoani Geita Katoni 328 za pombe bandia zanaswa mkoani Geita Reviewed by Zero Degree on 10/21/2019 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.