Loading...

Maadhimisho ya kumuenzi Mwl. Nyerere yafikia kilele Jumatatu


Leo ni siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka ishirini tangu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuaga dunia.

Maadhimisho haya yamefanyika Jumatatu kitaifa katika mkoa wa Lindi nchini Tanzania.

Katika kilele cha maadhimisho hayo vyombo vya habari vimeendelea kupeperusha baadhi ya hotuba za Mwalimu Nyerere alizozitoa wakati wa kupigania uhuru, akiwa madarakani na baada ya kustaafu uongozi.

Kwa upande wake Rais John Magufuli, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo amekaripia vitendo vya rushwa akitaka taasisi husika ziwachukulie hatua wote wanaokutikana na hatia.

Kadhalika wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania wameungana pamoja katika kumbukumbu hii ya muasisi wa taifa la Tanzania wakiangalia urithi aliowaachia kiongozi huyo baada ya kufariki dunia.

Ikiwa ni sehemu ya kumuenzi mwalimu kumekuwepo na makongamano yaliyoshirikisha viongozi wastaafu, wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida kupitia vyombo vya habari na katika majukwaa mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.

Naye Rais mstaafu Jakaya Kikwete akishiriki katika mjadala mojawapo alimtaja Mwalimu Nyerere kama mtu muungwana aliyejawa na ubinadamu.

Kikwete aliwasihi wanaotaka kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo basi wasiwe viongozi wa "kujimwambafai".

Msamiati huo ambao umeshika kasi nchini Tanzania unamaana ya kwamba kiongozi kutumia umwamba au mabavu.

Akizungumza kwenye kongamano moja kabla ya maadhimisho haya ya leo, mwanasiasa wa siku nyingi, Getruda Mongella alisema suala la ustawishaji wa demokrasi halipaswi kupuuziwa.
Maadhimisho ya kumuenzi Mwl. Nyerere yafikia kilele Jumatatu Maadhimisho ya kumuenzi Mwl. Nyerere yafikia kilele Jumatatu Reviewed by Zero Degree on 10/14/2019 03:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.