Loading...

Mambo yazidi kuwa magumu kwa Zinedine Zidane Real Madrid


KITENDO cha Real Madrid kupata sare tena ya kuitafuta kwa ‘tochi’ dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji katika Ligi ya Mabingwa Ulaya sasa ni rasmi kimemuweka pabaya Zinedine Zidane.

Real Madrid, mabingwa mara 13 wa michuano ya Ulaya walipata sare ya mabao 2-2 wakiwa nyumbani dhidi ya timu ambayo ilionekana ni ndogo kwao, kitendo ambacho kimewachukiza mashabiki wengi wa Madrid na kuamini kocha wao, Zidane sasa timu imemshinda.

Magazeti na vyombo vya habari vya Hispania vimeishambulia timu hiyo na hali inaonyesha kuwa kibarua cha Zidane kipo hatarini kwa kuwa wamekosoa hadi aina ya uchezaji wa timu kuwa ni mbovu.

“Wamevuruga Tena”, “Kengele imelia”, hivyo ni baadhi ya vichwa vya habari vya magazeti ya Hispania kuhusu Madrid. Ikumbukwe kuwa mechi iliyopita ya michuano hiyo, Madrid ilipigwa mabao 3-0 na Paris Saint-Germain.
Mambo yazidi kuwa magumu kwa Zinedine Zidane Real Madrid Mambo yazidi kuwa magumu kwa Zinedine Zidane Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 10/04/2019 07:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.