Loading...

Nchimbi ajumuishwa kikosini Stars baada ya kupiga 'Hat-trick' dhidi ya Yanga


Mshambuliaji Ditram Nchimbi wa klabu ya Polisi Tanzania ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kukamilisha wachezaji 29, kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda.

Nchimbi ameongezwa katika kikosi cha wachezaji 28, ambacho kilikuwa kimeshatajwa tayari. Hiyo imekuja baada ya kufunga magoli matatu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga jana jioni Oktoba 3, 2019.

Kocha Etienne Ndairagije ametaja kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kujiwinda na mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA utakaopigwa jijini Kigali Rwanda, Oktoba 14, 2019.

Katika mchezo dhidi ya Yanga, Nchimbi alifunga magoli matatu na kuisaidia timu yake kutoa sare ya 3-3 kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam.
Nchimbi ajumuishwa kikosini Stars baada ya kupiga 'Hat-trick' dhidi ya Yanga Nchimbi ajumuishwa kikosini Stars baada ya kupiga 'Hat-trick' dhidi ya Yanga Reviewed by Zero Degree on 10/04/2019 07:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.