Loading...

Nyoni aweka rekodi Stars ikifuzu CHAN


TIMU ya taifa ndiyo habari ya mjini kila kona ya nchi, ikiwa ni baada ya kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za michuano ya wachezaji wanaocheza Ligi ya ndani (CHAN), huku jina la Erasto Nyoni likiweka rekodi.

Hiyo inatokana na Nyoni kuwa chachu ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan juzi, nyota huyo alifunga bao kali la kusawazisha kipindi cha pili, akiweka rekodi ya kuwa mchezaji mkongwe pekee katika kikosi cha Stars.

Nyoni alikuwa sehemu ya kikosi hicho cha Etiene Ndayiragije, pia miaka 10 iliyopita alikuwewepo wakati Taifa Stars ilipofuzu mara mwisho ya kucheza fainali hizo.

Kikosi cha wakati huo ambacho kilicheza mechi kadhaa hadi kufuzu kikiwa chini ya kocha Márcio Máximo, makipa walikuwa ni Deogratius Boneventure ( Simba) Shaban Dihile ( JKT Ruvu), Farouk Ramadhan (Miembeni)

Mabeki: Shadrack Nsajigwa, Nadir Harob ‘Cannavaro’, Amir Maftar( Yanga), Kelvin Yondani ‘ Vidic’, Juma Jabu ( Simba) na Salum Swed (Mtibwa), Erasto Nyoni, Salvatory Ntebe (Azam FC).

Viungo: Nurdin Bakari, Godfrey Bonny, Abdi Kassim, Athuman Idd ‘Chuji’ ( Yanga) Shaban Nditi, Zahoro Pazi ( Mtibwa Sugar) Nizar Khalfan ( Moro United), Haruna Moshi ‘Boban’ Henry Joseph na Jabil Aziz ( Simba) na Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).

Washambuliaji waliongozwa na Mrisho Ngassa, Jerry Tegete na Kigi Makasi( Yanga) Uhuru Seleman ( Mtibwa) na Mussa Hassan Mgosi ( Simba).
Nyoni aweka rekodi Stars ikifuzu CHAN Nyoni aweka rekodi Stars ikifuzu CHAN Reviewed by Zero Degree on 10/21/2019 07:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.