Loading...

Tembo zaidi ya 50 wafa kwa kukosa maji ya kunywa

Baadhi ya tembo hao walipatikana karibu na maeneo ya maji

Tembo 55 wamekufa njaa katika mbuga ya kitaifa ya Hwange, nchini Zimbabwe kutokana na ukame mkali uliokithiri kwa zaidi ya miezi miwili.

"Hali ni mbaya," Msemaji wa mbuga hiyo Tinashe Farawo, anasema. "Tembo wanakufa kutokana na ukame na hili ni tatizo kubwa."

Ukame umepunguza kwa kiwango kikubwa viwango vya mimea nchini Zimbabwe.

Theluthi moja ya watu nchini humo wameripotiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula wakati mgogoro wa kiuchumi ukiendelea nchini humo.

Mwezi Agosti, ripoti ya Shirika la Chakula Duniani ilisema kuwa watu milioni mbili wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.

Baadhi ya tembo walipatikana katika eneo la mita 50 (yadi) ya maji -kuashiria kuwa walitembea mwendo mrefu bila maji na hatimaye kufa muda mfupi kabla ya kuyafikia.

Tembo hao wamesababisha "uharibifu mkubwa" wa mimea katika mbuga ya Hwange, Bw. Farawo alisema.

Mbuga hiyo inawahifadhi karibu tembo 15,000 lakini kwa sasa kuna zaidi ya tembo 50,000.

Mbuga ya Hwange ambayo haijakuwa ikipokea ufadhili kutoka kwa serikali - imekuwa ikijaribiu kuchimba visima lakini inakabiliwa na changamoto ya fedha ya kuendelea na mradi huo, Bwana Farawo aliongeza kusema.

Mizoga ya tembo hao ilipatikana katika mashimo ya maji yaliyokauka.
Tembo zaidi ya 50 wafa kwa kukosa maji ya kunywa Tembo zaidi ya 50 wafa kwa kukosa maji ya kunywa Reviewed by Zero Degree on 10/22/2019 07:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.