Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Oktoba 8, 2019


Solskjaer anahitaji kitita cha £300m kutumia katika dirisha lijalo la uhamisho na kumnunua mshambuliaji kama vile mshambuliaji wa Tottenhama na Uingereza Harry Kane,26, kulingana na winga wa zamani Lee Sharpe. (Talksport)

Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anahofia kwamba hatma ya kazi yake itakuwa haijulikani iwapo timu yake itashindwa kwa mabao mengi ugenini Liverpool.(Mail)

Baadhi ya wachezaji wamepoteza matumaini na raia huyo wa Norway anaamini baadhi yao wamekataa kumsikiliza. (Sun)

Kane anafaa kuondoka Tottenham na badala yake kuhamia Manchester City, kulingana na beki wa zamani wa England Glen Johnson. (Betdaq)

Mshambulaji wa Arsenal Gabriel Martinelli, 18, anakabiliwa na chaguo katika hatma yake ya kimataifa kwa kuwa anahitajika na Itali pamoja na Brazil. Alizaliwa nchini Brazil lakini lakini babake ni raia wa Itali hivyobasi anaweza kuwakilisha timu zote mbili.

Liverpool huenda ikapokea kitita cha £4.5m kati ya kile cha £84m wanazodaiwa na Barcelona baada ya kumnunua kiungo Philippe Coutinho, 27, ambaye alihamia Nou Camp mwaka 2018. (Mirror)

Everton inafikiria kumnunua mchezaji anayelengwa na Manchester United Moussa Dembele katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa , mwenye umri wa miaka 23 anaweza kugharimu £40m kutoka Lyon. (Star)

Christian Pulisic, 21


Mshambuliaji wa klabu ya 
Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 21, amekiri kukasirishwa kwake kwa kukosa muda wa kucheza zaidi tangu uhamisho wake wa £58m kutoka Borussia Dortmund. (Guardian)

Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, 30, amekiri kwamba angependelea kuandikisha mkataba wa kudumu na klabu ya Newcastle lakini akasema kwamba hakupatiwa fursa kubadili uhamisho wake wa mkopo wa msimu uliopita kuwa kandarasi ya kudumu na hivyobasi akaelekea katika klabu ya China ya Dalian Yifang. (Newcastle Chronicle)

Mkufunzi Roy Hodgson anasema kwamba klabu ya Crystal Palace italazimika kumsaini mshambuliaji mpya mwezi januari iwapo wanataka kumaliza katika orodha ya timu sita za kwanza katika jedwali na pia analenga kuwasajili mabeki wawili wapya wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. (Standard)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Oktoba 8, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Oktoba 8, 2019 Reviewed by Zero Degree on 10/08/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.