Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Oktoba 22, 2019
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, anasema kuwa anahofia kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya klabu hiyo (Mirror)
Juventus na Atletico Madrid zinamfuatilia beki wa West Brom wa miaka 19, Nathan Ferguson.
Beki wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Sol Campbell, 45, anafanya mazungumzo ya kuwa mkufunzi wa Southend, inayoshiriki soka la daraja ya kwanza - miezi miwili baada ya klabu ya Macclesfield inayocheza soka ya daraja la pili. (Sun)
Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 22, anakaribia kutia saini mkataba mpya wa kusalia Stamford Bridge baada ya kufunga mabao manane katika ligi ya Premia msimu huu.
Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, anatakiwa na Crystal Palace na huenda akajiunga na klabu hiyo ifikapo mwezi Januari. (Daily Star)
Real Madrid haitajaribu kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham raia wa Denmark, Christian Eriksen, 27, mwezi Januari hadi watakapowauza wachezaji wasiokuwa katika kikosi cha kwanza. (AS)
![]() |
| Christian Eriksen, 27 |
Barcelona imemaliza mzozo wake na Atletico Madrid kuhusu usajili wa Antoine Griezmann, 28, kwa kumlipia euro milioni 15 zaidi mshambuliaji huyo wa Ufaransa. (El Mundo)
Derby itampatia nahodha wa zamani wa England Wayne Rooney, 33, mafunzo maalum kuhakikisha yuko tayari kwa mashindano atakapojiunga na klabu hiyo kutoka DC United.
Derby itampatia nahodha wa zamani wa England Wayne Rooney, 33, mafunzo maalum kuhakikisha yuko tayari kwa mashindano atakapojiunga na klabu hiyo kutoka DC United.
Arsenal inaongoza katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa RB Leipzig na Ufaransa wa chini ya miaka-21 Dayot Upamecano, 20, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni 50. (Mail)
Kiungo wa kati wa Brazil na Manchester United Fred, 26 - ambaye alinunuliwa kwa kima cha £47m kutoka Shakhtar Donetsk mwezi Juni 2018 - anaamini kuwa ameanza kupata uzoefu wa soka la Uingereza. (Telegraph)
Meneja wa Italia Roberto Mancini huenda akamjumuisha kipa mkongwe wa Juventus Gianluigi Buffon, 41, na kiungo wa kati wa Boca Juniors wa miaka 36 Daniele de Rossi katika kikosi cha Euro 2020. (Rai Sport via Mail)
Kiungo wa kati wa Brazil na Manchester United Fred, 26 - ambaye alinunuliwa kwa kima cha £47m kutoka Shakhtar Donetsk mwezi Juni 2018 - anaamini kuwa ameanza kupata uzoefu wa soka la Uingereza. (Telegraph)
Meneja wa Italia Roberto Mancini huenda akamjumuisha kipa mkongwe wa Juventus Gianluigi Buffon, 41, na kiungo wa kati wa Boca Juniors wa miaka 36 Daniele de Rossi katika kikosi cha Euro 2020. (Rai Sport via Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Oktoba 22, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
10/22/2019 08:05:00 AM
Rating: