Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Oktoba 5, 2019


Barcelona wanaweza kumtumia Antoine Griezmann kufanikisha dili la kumpata Neymar kwenye kipindi kijacho cha majira ya joto, huku dalili zikionyesha kuwa mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa bado hajapatana vizuri na Lionel Messi.

Rangers wanatarajiwa kumteua Ross Wilson wa Southampton kama mkurugenzi wao mpya wa kandanda miaka miwili ikiwa imepita baada ya kukataa kwenda katika dimba la Ibrox. (Daily Mail)

Mlinzi wa zamani wa Tottenham na Arsenal Sol Campbell na mshambuliaji wa zamani wa Celtic na Barcelona Henrik Larsson wamehojiwa kuchukua wadhifa wa meneja wa klabu ya Southend.

Mario Mandzukic na Callum Wilson wanaongoza orodha ya wachezaji ambao wanawaniwa na klabu ya Manchester United.

Nyota wa Chelsea Callum Hudson-Odoi amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo ya London. (Sky Sports)

Chelsea inamatumaini kuwa mlinzi wake Fikayo Tomori, 21, na mshambuliaji Tammy Abraham, 22, watasaini mkataba mpya wiki chache zijazo.

Wachezaji hao wawili wamejumuishwa katika kikosi timu ya taifa ya Uingereza cha kufuzu kwa kintang'anyuro cha Euro 2020 baadae mwezi huu. (Standard)

Sir Alex Ferguson atamfuatlia kwa karibu kiungo wa klabu ya Aston Villa John McGinn - kabla ya kumpendekeza Mskoti huyo kwa wakurugenzi wa klabu ya Manchester United.

Jamaa wa Peter Kenyon wamerejea na ofa yao ya pauni milioni 300 kuinunua klabu ya Newcastle kwa kusajili kampuni mpya itakayosimamia mazungumzo hayo.

Aleksandr Sobolev


Ole Gunnar Solskjaer amemwongeza mshambuliaji wa Krylia Sovetov Aleksandr Sobolev kwenye orodha ya washambuliaji anaolenga kuwasajili.

Mkufunzi wa klabu ya River Plate Marcelo Gallardo yuko mstari wa mbele kuchukua nafasi ya Ernesto Valverde, ambaye msimu huu anaoneka kuwa na wakati mgumu katika klabu ya Barcelona. (Sun)

Manchester United inamsaka mshambuliaji wa Urusi Aleksandr Sobolev, 20 ayechezea klabu ya PFC Krylia Sovetov Samara ya Ligi Kuu ya Urusi.

Tottenham wamemfanya James Maddison kuwa chaguo lao la kwanza kuchukua nafasi ya Christian Eriksen.

Lionel Messi anaweza akakumbuna na vikwazo vya kusafiri kwenda Umoja wa Ulaya (UK) kama Barcelona ijiweka upande wa Uingereza kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya Brexit.

Alisson anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Liverpool kwenye mchezo wao dhidi ya Leicester Jumamosi.

Mkataba wa klabu ya Liverpool na kampuni ya Nike, utawashuhudia vigogo hao wa Amerika wakiwatumia watu kama Drake, Serena Williams na LeBron James kuitangaza klabu hiyo. (Mirror)

Chelsea wataanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na Willian, huku meneja wa klabu hiyo Frank Lampard akiwa na matamanio makubwa ya kumbakisha winga huyo.

Manchester United wanalenga kumsajili nyota wa timu ya taifa ya Mexico Jose Juan Macias, ambaye anafananishwa na Javier Hernandez. (Express)

Klabu ya Manchester City haina mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Norway mwenye umri wa miaka 20 Martin Odegaard, ambaye yuko Real Sociedad kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Manchester Evening News)

Joao Cancelo


Pep Guardiola amemuonya Kyle Walker kwamba nafasi yake katika kikosi cha Manchester City inawezakuwa shakani ikiwa Joao Cancelo ataendelea kuonyesha kiwango kizuri. (Times)

Loris Karius anatarajia kuichezea Liverpool kwa mara nyingine tena baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo na klabu ya Besiktas. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Oktoba 5, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Oktoba 5, 2019 Reviewed by Zero Degree on 10/05/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.