Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Oktoba 9, 2019


Mshambuliaji raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, amesema hakuwa na mpango wa kuondoka Juventus msimu huu licha ya kuhusishwa na uhamisho kuelekea vilabu vya Manchester United na Tottenham. (Tuttosport)

Kuna uwezekano Manchester United ikashuka daraja msimu huu, kwa mujibu wa kocha wa zamani wa Uingereza, Sam Allardyce. (Talksport)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atafutwa kazi endapo timu yake itafungwa na Norwich mwishoni mwa mwezi, ripoti zinaeleza. (Sun)

Hata hivyo, vyanzo vingine vinaarifu kuwa uongozi wa klabu ya Manchester United upo tayari kumvumilia na kumpa muda zaidi Solskjaer wa kufanya mageuzi klabuni, licha ya kiwango kibovu cha matokeo ya mwanzo wa msimu kwa miaka 30. (Telegraph)

Kiungo wa Arsenal Dani Ceballos, 23, amesema alaifanya uamuzi sahihi kujiunga na 'the Gunners' kwa mkopo akitokea Real Madrid baada ya kuitwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania.

United wanapanga kuwasajili kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 20, na beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, bila kujali mustakabali wa Solskjaer. (Goal)

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anapanga kuwauza wachezaji kadhaa wa klabu hiyo baada ya kuanza msimu kwa kiwango kibovu. Wachezaji watakaowekwa sokoni mwezi Januari ni; Eric Dier, 25, Christian Eriksen, 27, Serge Aurier, 26, Victor Wanyama, 28, pamoja na Danny Rose, 29. (Times)

Kocha David Moyes yupo tayari kurudi kuifunza klabu yake ya zamani ya Everton, katika kipindi ambaco kocha wa sasa Marco Silva akiwa katika shinikizo kubwa baada ya timu hiyo kuwa chini ya mstari wa kushuka daraja. (Mirror)

Crystal Palace watalazimika kulipa pauni milioni ili 22 wamsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, ambaye yupo kwa mkopo Palace toka Januari mwaka huu. (Express)

Klabu ya Barcelona itampatia kipa wake Mjerumani Marc-Andre ter Stegen, 27, mkataba wa muda mrefu hivi karibuni. (Marca)

Mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Kevin Phillips anataka kuchukua nafasi ya ukocha wa timu hiyo baada kufutwa kazi kwa kocha Jack Ross. (Star)

Borussia Dortmund wameungana na Arsenal, Juventus na Paris St-Germain katika kufuatilia maendeleo ya winga kinda wa Celtic ya Uskochi, Karamoko Dembele, mwenye miaka 16. (Bild)

Lyon inatarajiwa kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na Paris St-Germain Laurent Blanc baada ya kumtimua kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Sylvinho. (L'Equipe)

Shkodran Mustafi, 27


Beki wa kati wa Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi, 27, amekasirishwa vikali na kura ya maoni iliyoendeshwa na gazeti la Uhispania la Marca ambapo ametajwa kuwa beki namba mbili mbovu zaidi duniani baada ya Phil Jones wa Man United.

Ushiriki wa klabu za Ligi ya Primia ya England katika michuano ya Champions League utapunguzwa kutoka timu nne zinazofuzu moja kwa moja mpaka timu tatu, chini ya mapendekezo mapya ya kanuni za mashindano. (Mail)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Oktoba 9, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Oktoba 9, 2019 Reviewed by Zero Degree on 10/09/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.