Loading...

Watanzania watuombee tufanye vizuri - Kaseja

Juma Kaseja

Kuelekea mchezo wa kirafiki leo dhidi ya Rwanda, nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja, amesema mchezo huo utatoa picha kamili kwa kocha wa kikosi hicho Etienne Ndayiragije kuelekea mchezo wa CHAN dhidi ya Sudan.

Akiongea kwenye mahojiano kabla ya mchezo jijini Kigali, Kaseja amesema wao wameshafanya maandalizi yote lakini wanaamini mwalimu atakuwa anatazama zaidi mchezo ujao.

''Mimi nafikiri mchezo utampa nafasi kocha wetu kujua tunaingiaje kwenye mchezo dhidi ya Sudan hiyo Oktoba 18, 2019, sisi tumejiandaa vizuri nawaomba tu watanzania watuombee tufanye vizuri', - amesema.

Kwa upande wake kocha msaidizi Suleiman Matola amesema kuwa wanauchukulia kwa umuhimu wote mchezo huo, na kwamba kwasababu unapigwa siku ya kumuenzi Baba wa taifa, watafanya kila namna ili kushinda mchezo huo.
Watanzania watuombee tufanye vizuri - Kaseja Watanzania watuombee tufanye vizuri - Kaseja Reviewed by Zero Degree on 10/14/2019 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.