Wingu zito wizi wa kompyuta katika ofisi ya DPP
Kulingana na taarifa ya Habari Leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo, jana Kamanda huyo hakuwa tayari tena kuzungumzia suala hilo.
Hali kadhalika DPP, Biswalo Mganga naye kwa siku ya pili jana hakuweza kujitokeza kuzungumzia kuhusiana na mkasa huo ulioibua hisia tofauti tofauti miongoni mwa Watanzania hasa katika kipindi hiki ambacho ofisi yake imekuwa inashughulikia maombi ya misamaha kutoka kwa washitakiwa wa kesi za uhujumu uchumi.
Taarifa hiyo inadai kuwa kwa siku nzima jana, simu ya mkononi ya DPP ilikuwa inaita bila kupokelewa kwa zaidi ya mara nne wakati mwandishi alipokuwa anampigia ili kupata ufafanuzi wa kina wa tukio hilo.

Kwa upande wa Kamanda Mambosasa ambaye juzi alikiri kutokea kwa wizi huo, jana alipoulizwa kama kuna watu wanaoshikiliwa na jeshi hilo kutokana na wizi huo hadi sasa, alisema hana taarifa kama kuna mtu anashikiliwa.
Baada ya kuhojiwa, Kamanda Mambosasa alitumia chini kidogo ya dakika moja kutoa jibu…”naingia kwenye kikao, sijui kama kuna aliyekamatwa sina taarifa,” kisha simu ilikatika.
Tofauti na ilivyozoeleka yanapotea matukio makubwa kama hayo ambapo Jeshi la Polisi hufanya mkutano na waandishi wa habari mara moja kutoa ufafanuzi wa kina, tukio hilo la wizi wa kompyuta bado limeeendelea kugubikwa na giza totoro.
Juzi Kamanda Mambosasa alithibitisha kutokea kwa wizi huo wa kompyuta, katika tukio alilosema lilitokea Oktoba 15, mwaka huu majira ya asubuhi.
Wizi huo umeonekana kugusa hisia za watu wengi hasa ikizingatiwa kuwa umetokea kipindi ambacho ofisi hiyo iko katika mchakato wa kujadiliana na kuingia makubaliano na washitakiwa mbalimbali wa kesi za uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha na kurejesha fedha walizohujumu.
Taarifa zaidi ambazo hazikuweza kuthibitishwa na ama DPP ama Jeshi la Polisi, zimeeleza kuwa baadhi ya watumishi wa ofisi ya DPP wapo mikononi mwa polisi wakifanyiwa mahojiano ya kina kuhusiana na tukio hilo.
Habari hizo zimesema simu za mikononi za baadhi ya watumishi hao wa ofisi ya DPP zinashikiliwa kwa uchunguzi zaidi ili kubaini mazingira yaliyowezesha wizi huo kufanyika.
Wingu zito wizi wa kompyuta katika ofisi ya DPP
Reviewed by Zero Degree
on
10/21/2019 12:50:00 PM
Rating: