Loading...

Yanga yapangiwa Waarabu CAF


KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam imepangwa kucheza dhidi ya Pyramids FC ya Misri katika mechi ya kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho usiku wa kuamkia leo.

Yanga itaanza mechi yake ya kwanza nyumbani Oktoba 27, 2019 kabla ya kurudiana Misri Novemba 3, 2019 ambapo mshindi wa mchezo huo anafuzu moja kwa moja kwa hatua ya makundi.

Pyramids FC inayofundishwa na kocha wa zamani wa Uganda, Mfaransa Sebastien Desabre, ilifuzu kwa hatua hiyo baada ya kuing’oa Belouizdad katika raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1.

Ratiba kamili
  • Horoya (Guinea) Vs Bandari (Kenya)
  • Young Africans (Tanzania) Vs Pyramids (Egypt)
  • Enyimba (Nigeria) Vs TS Galaxy (South Africa)
  • Zamalek (Egypt)/Generation Foot (Senegal) Vs ESAE (Benin)
  • Asante Kotoko Vs San Pedro (Cote d’Ivoire)
  • KCCA (Uganda) Vs Paradou (Algeria)
  • Gor Mahia (Kenya) Vs DC Motema Pembe (DR Congo)
  • UD Songo (Mozambique) Vs Bidvest Wits (South Africa)
  • Elect Sport (Chad) Vs Djoliba (Mali)
  • Green Eagles (Zambia) Vs HUSA (Morocco)
  • Cano Sports (Equatorial Guinea) Vs Zanaco (Zambia)
  • Fosa Juniors (Madagascar) Vs RS Berkane (Morocco)
  • Cote d’Or (Seychelles) Vs Al Masry (Egypt)
  • ASC Kara (Togo) Vs Rangers (Nigeria)
  • FC Nouadhibou (Mauritania) Vs Triangle United (Zimbabwe)
  • El Nasr (Libya) Vs Proline (Uganda)
Yanga yapangiwa Waarabu CAF Yanga yapangiwa Waarabu CAF Reviewed by Zero Degree on 10/10/2019 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.