Serikali kuajiri walimu 16000
Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Novemba 14, 2019, Bungeni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya moja kwa moja kutoka kwa wabunge na kuongeza kuwa si upande wa elimu pekee, bali pia wataajiri wauguzi na wahudumu wa afya ili kuboresha huduma hizo kwani serikali imeshafanmikiwa kujenga hospitali na zahanati nchi haopa nchini kipindi kifupi hivyo zinahitaji watumishi.
“Serikali imeanza kutoa vibali vya ajira kwenye sekta za Afya, Elimu na Kilimo, na tunakaribia kutoka vibali kwa ajili ya kuajiri walimu 16000 kwa upande wa Elimu za Msingi na Sekondari, vilevile tutatoa vibali vya ajira katika sekta ya afya.
“Ununuzi wa korosho msimu 2019/20 utatumia mfumo uleule wa ushirika kwa njia ya minada. Serikali itahakikisha wanunuzi wanalipa vyama vya ushirika kwa wakati na vyama vya ushirika vinawalipa wakulima ndani ya siku saba. Mpaka sasa hali ni shwari.”- PM Kassim Majaliwa.
“Tunataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme ifikapo 2021, kazi hiyo inaendelea vizuri na inasimamiwa vizuri na Wizara ya Nishati. Rais Magufuli amepunguza bei kuhakikisha wananchi wanamudu, bei ya kuunganishwa ni Tsh 27,000 tu.
“Viongozi walio katika maeneo yenye upungufu wa chakula kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya, wawasilishe taarifa zao kwa wizara ya husika ili kuona namna ya kusaidia,” amesema Majaliwa.
Spika wa Bunge Job Ndugai leo amemkatalia mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Devotha Minja kumuuliza swali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa maelezo kuwa kanuni za Bunge zinakataza mbunge kuandaliwa swali na kulisoma bungeni.
Serikali kuajiri walimu 16000
Reviewed by Zero Degree
on
11/14/2019 09:05:00 AM
Rating: