Wanasayansi waelezea chanzo cha virusi vya Corona
Wanasayansi walipinga uvumi kwamba virusi hivyo huenda vilitengenezewa katika maabara |
Mlipuko wa virusi vya corona ambao umewawacha zaidi ya watu milioni moja wakiwa wameambukizwa na wengine 60,000 wakiwa wamefariki umebadilisha ulimwengu ulivyokuwa.
Na pengine kwasababu ya athari yake kubwa umezua msururu wa nadharia zilizozuka punde baada ya visa vya kwanza kutangazwa nchini China mapema mwezi Januari.
Wengi wao wanaangazia nadharia mbili: Ya kwanza ni kwamba virusi hivyo vya corona vilitengenezwa katika maabara moja ya China na kusambazwa kama silaha ya kibaiolojia dhidi ya mataifa yenye uwezo mkubwa.
Wengi wao wanaangazia nadharia mbili: Ya kwanza ni kwamba virusi hivyo vya corona vilitengenezwa katika maabara moja ya China na kusambazwa kama silaha ya kibaiolojia dhidi ya mataifa yenye uwezo mkubwa.
Na sababu ya pili ni kwamba kirusi hicho kilifanikiwa kutoroka kutokana na uzembe wa watafiti wa China na hivyobasi kuanza kusambaa kote duniani.
Wale wanaowatetea wanasema kwamba kuna virusi vinavyotengezwa na chemikali kwa lengo la kufanyiwa utafiti wa kisayansi na kwamba hapo kale vimekuwa vikivuja katika maabara zinazodaiwa kuwa na usalama wa hali ya juu.
Wale wanaowatetea wanasema kwamba kuna virusi vinavyotengezwa na chemikali kwa lengo la kufanyiwa utafiti wa kisayansi na kwamba hapo kale vimekuwa vikivuja katika maabara zinazodaiwa kuwa na usalama wa hali ya juu.
Virusi vya SARS-CoV-2 havikuanzishwa katika maabara bali vilitokana na asili |
Pia mjini Wuhan , ambao ndio chanzo cha mlipuko wa virusi hivyo kuna taasisi inashughulikia maambukizi ya virusi ambayo inaweza kudhibiti virusi kadhaa vinavyoweza kusababisha maafa na ipo karibu na soko ambalo virusi hivyo vinadaiwa kuanzia.
Kundi moja la wanasayansi limekataa uvumi
Watafiti walifanikiwa kubaini kwamba SARS-CoV-2 jina la kirusi kinachosababisha virusi vya corona hakikutengezwa na mwanadamu na badala yake kilitokana na asilia.
''Tulifanikiwa kubaini jeni za virusi hivyo vipya kamba havikutengezwa katika maabara na badala yake ni bidhaa ya asilia'', Dkt Robert E Garry, profesa katika chuo kikuu cha Tulane nchini marekani na mojawapo ya kundi la utafiti huo.
''Nadharia hii inafutilia mbali uvumi kwamba virusi vya corona ni silaha ya kibaiolojia iliotengezwa na mwanadamu'', aliongeza.
''Tuliweza kubaini kwamba haiwezekani kwa mtu yeyote kutengeneza virusi hivi katika maabara'', aliongezea.Na ili kufikia uamuzi huo walilazimika kuangazia jeni za virusi hivyo na kulinganisha na virusi vilivyopo katika maabara ya kukabiliana na virusi.
Ramani ya Jeni
Wakati wa kuanza kwa mlipuko huo kulikuwa na hali ya switofahamu .
Haikubainika kwa haraka ni nini kilichokuwa kinasababisha ugonjwa wa mapafu uliokuwa hatari miongoni mwa makumi ya wagonjwa nchini China.
Baadaye hilo likabainika kwamba kilikuwa kirusi kipya cha SARS-CoV-2. Lakini je kilikuwa kinatoka wapi?.
Kama ilivyoelezwa na kundi hilo la utafiti , lililoongozwa na mtaalamu wa mgonjwa ya maambukizi Kristian Andersen na wataalam kutoka mataifa tofauti,
Lengo lao kutoka mwanzo lilikuwa kufutilia mbali uvumi uliokuwa ukienea kwamba mlipuko huo ulianzishwa na mwanadamu.
Kirusi cha karibu na kile cha Covid 19 kinatokana na popo .. Ukweli ni kwamba virusi vya popo ni asilimia 96 sawa na vile vya SARS-Cov-2.
''Sio rahisi kukamilisha tofauti iliopo katika maabara'' , aliongezea mwanasayansi huyo.
Baada ya uchunguzi uliofanywa na watafiti , kundi hilo liliafikika uamuzi kwamba kirusi hicho kipya kilikuwa na chanzo asilia kulingana na matokeo ya utafiti huo yaliochapiswa chini ya kichwa kikuu ''An Aproach to the Origin of SARS CoV-2'' katika jarida la tiba asilia la mwezi Machi.
''Tulilinganisha virusi vyote vikiwemo vile ambavyo vilikuwa vinaweza kupatikana kutoka kwa pangolin na popo na hesabu za tarakilishi zilibaini kwamba kirusi kilichokuwa na uwezo wa kuambukiza na kufanya madhara makubwa hakiwezi kuwa kiliundwa katika maabara'', alielezea.
Kwa mtaalamu huyo na kundi lake , mbali na kufutilia mbali uvumi uliokuwa ukisambaa kuhusu chanzo na lengo la virusi hivyo , matokeo ya ripoti hiyo pia ilikuwa kuonyesha jinsi virusi hivyo hukua.
''Sasa tumegundua kwamba kuna njia mpya kutengeneza virusi vya corona vinavyoweza kuambukiza wanadamu ambavyo ni mchanganyiki wa virusi viwili asilia'', alisema Garry.
"Tayari tunajua kwamba virusi vya SARS-CoV na MERS - ni virusi vingine vinavyosababisha matatizo ya mtu kuweza kupumua - na huambukizwa kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu bila mabadiliko.
''Pia tunajua kuwa virusi vya coronavirus katika wanyama vinaweza kusababisha janga '', kama ilivyo sasa , alielezea.
Na alihitimisha: "Kuonyesha tabia ya virusi vya corona katika wanyama kama vile popo ni kipaumbele."
Chanzo: BBC
Wanasayansi waelezea chanzo cha virusi vya Corona
Reviewed by Zero Degree
on
4/09/2020 10:50:00 AM
Rating: