Loading...

Mwenyekiti atishia kujiuzulu Shinyanga

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje.


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje ,ametishia kujiuzuru nyadhifa hiyo, kwa madai ya kutoheshimiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nice Munissy.

Mboje akizungumza leo kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Salawe, na Madarasa matatu katika Shule mpya ya Sekondari Mhangu iliyopo Salawe.

Amesema kwenye Halmashauri hiyo tangu aingie Mkurugenzi huyo mpya hakuna tena kuheshimiana wala maelewano mazuri, na hivyo kuona ni bora aachie ngazi ya uenyekiti ili abaki kuwatumia wananchi wake wa Kata ya Mwalukwa.

"Tangu 2011 nipo kwenye Halmashauri hii, na Wakurugenzi wote waliopita walikuwa wakini heshimu, lakini sasa hivi hakuna heshima, ni bora nikachukua maamuzi ya kuachia ngazi ya uenyekiti nibaki na udiwani wangu kutumikia wananchi," amesema Mboje.

Aidha, katika ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa wakati wa kutembelea miradi ya maendeleo, Mwenyekiti huyo alikuwa akilalamika kuwa amenyimwa gari na Mkurugenzi, sababu ya kutomheshimu, na hivyo kulazimika kupanda kwenye gari la chama.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nice Munissy, akizungumzia suala la Magari, amesema Halmashauri hiyo ina Magari 24, lakini Magari Sita ndiyo yanafanya kazi, na yaliyosalia yote ni Mabovu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema ,alimtaka Mwenyekiti huyo wa Halmashauri asiwe Mnyonge, bali kama kuna mapungufu amwite Mkurugenzi wakae wamalize changamoto zao.

Pia, amesema kama haiwezekani amwite kwenye Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,ili wapate kusuluhishwa, sababu kama Mwenyekiti na Mkurugenzi hawana maelewano mazuri, Halmashauri hiyo haiwezi Songambele kimaendeleo.

Chanzo: Nipashe
Mwenyekiti atishia kujiuzulu Shinyanga Mwenyekiti atishia kujiuzulu Shinyanga Reviewed by Zero Degree on 11/03/2021 10:31:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.