Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Aprili, 2024

Michael Olise, 22

Winga wa Crystal Palace Mfaransa Michael Olise, 22, atakuwa tayari kuhamia Manchester United msimu ujao.

Arsenal na Manchester City wamefahamishwa kuwa Newcastle United wako tayari kusikiliza ofa zinazozidi thamani ya £80m kwa kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 26, msimu huu ujao. (90min)

Manchester United itamlenga beki mpya wa kati, kiungo wa kati na mshambuliaji katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, huku mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 28, akiwa miongoni mwa wachezaji ambao hawapo tena katika mipango ya klabu hiyo.

Manchester United wana imani dau la kati ya £60-70m litatosha kumsajili beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, kabla ya Juni 30, na hivyo kuiruhusu Everton kujumuisha ada hiyo katika akaunti zao za 2023-24 na kuepuka kukatwa pointi zaidi. (Football Insider)

Meneja wa Wolves Gary O'Neil huenda akasaini mkataba mpya huko Molineux licha ya ripoti zinazomhusisha na kazi ya Liverpool.

Klabu ya Manchester United wanaweza kuanza kusaka usajili wa beki wa kushoto wa Uhispania Miguel Gutierrez, 22, kutoka Girona lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal na West Ham . (GiveMeSport)

Kifungu cha kutolewa cha Guimaraes cha pauni milioni 100 kitaanza kutumika kwa mwezi mmoja pekee, kuanzia mwishoni mwa Mei hadi mwishoni mwa Juni. (Fabrizio Romano)

Meneja wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer na mkufunzi wa zamani wa Leeds United Jesse Marsch wamewasiliana na Canada kuhusu kuiongoza timu ya taifa katika Kombe la Dunia la 2026.

Klabu ya Arsenal wanafuatilia wachezaji wengi wanaolengwa katika safu ya kati huku kukiwa na wasiwasi kwamba mkataba wa kiungo wa kati wa Real Sociedad na raia wa Uhispania Martin Zubimendi, 25, unaweza kuwa mgumu kufikiwa.(Standard)

Zubimendi anasema ripoti zinazomhusisha na baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya "ni uvumi tu" na ana furaha Real Sociedad. (Marca)

Ajax wana nia ya kumteua meneja wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter, ambaye pia yuko kwenye orodha ya Manchester United ya watu wanaoweza kuchukua nafasi ya Erik ten Hag. (Guardian)

Potter amekataa ofa ya kwanza kutoka kwa Ajax kwa sababu mshahara uliopendekezwa haukukidhi matarajio yake. (Het Parool)

Andriy Lunin, 25

Klabu ya Manchester United, Paris St-Germain na Bayern Munich zote zinavutiwa na mlinda mlango wa Real Madrid raia wa Ukrain Andriy Lunin, 25. (Fichajes)

Napoli wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili fowadi wa Canada Jonathan David, 24, kutoka Lille. (Calciomercato)

Klabu ya Bundesliga Stuttgart iko tayari kufanya uhamisho wa fowadi wa Ujerumani Deniz Undav, 27, kuwa wa kudumu baada ya kumsajili kwa mkopo kutoka Brighton msimu uliopita wa majira ya joto. (Caught Offside)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/26/2024 11:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.