Loading...

Wafungwa watoroka baada ya mvua kuharibu gereza


Zaidi ya wafungwa 100 wametoroka jela karibu na mji mkuu wa Nigeria baada ya mvua kubwa kuharibu sehemu waliyokuwa wakihifadhiwa.

Kwa mujibu wa mamlaka, wafungwa 118 awali walikimbia Gereza la Suleja lakini 10 wamekamatwa.

Msako umeanzishwa ili kuwatafuta wengine. Utambulisho wa wafungwa hao haujabainika kufikia sasa lakini kuna hofu kuwa baadhi yao wanaweza kuwa hatari.

Hata hivyo taarifa kutoka katika gereza hilo ilisema wanafanya kazi na vyombo vingine vya usalama na kwamba watu wanapaswa kuendelea na shughuli zao za kawaida bila hofu yoyote.

"Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama [sisi] kufikia sasa tumefanikiwa wakamata wafungwa 10 waliokuwa wakitoroka na kuwaweka chini ya ulinzi, huku tukiendeleza msako mkali wa kuwakamata wengine," ilisema taarifa kutoka kwa mamlaka ya magereza ya Abuja.

Iliongeza kuwa vituo vingi vya magereza huko Suleja, kilomita 50 kutoka Abuja vilijengwa wakati wa ukoloni na hivyo vimezeeka na ni dhaifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wafungwa watoroka baada ya mvua kuharibu gereza Wafungwa watoroka baada ya mvua kuharibu gereza Reviewed by Zero Degree on 4/26/2024 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.