Loading...

Intaneti yasababisha kufungwa kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania


Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umefungwa kwa siku mbili kutokana na ukosefu wa mtandao wa intaneti iliyoathiri nchi kadhaa za Afrika Mashariki.

"Kwa sababu ya huduma duni za mtandao kote nchini, ubalozi hautafunguliwa kwa umma," ubalozi ulisema kwenye chapisho kwenye X (zamani Twitter) siku ya Jumatatu.

Ubalozi huo umeahirisha miadi yote ya konsula kwa siku ya Jumanne na Jumatano hadi mambo yatakapotengamaa.

Ubalozi huo, hata hivyo, utaendelea kupatikana kwa makusanyo ya visa na kushughulikia kesi za dharura zinazohusisha raia wa Marekani.

Mtandao uliyopotea tangu Jumapili asubuhi, umesababisha umeathiri huduma za intaneti nchini Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda.

Tathmini ya kampuni ya ufuatiliaji wa mtandao ya NetBlocks siku ya Jumatatu ilionyesha kuwa Tanzania imeathirika zaidi na kukatika kwa huduma za intaneti.

Hitilafu hiyo imetokana na kukatika kwa nyaya za chini ya bahari zinazounganisha eneo hilo na dunia nzima kupitia Afrika Kusini, mtaalam wa sekta hiyo Ben Roberts aliambia BBC.

Siku ya Jumatatu, watu katika mataifa ya Afrika Mashariki walikuwa bado wanafikia kiasi kidogo sana cha mtandao huku baadhi ya watoa huduma za mawasiliano wakionyesha kuwa suala hilo lilikuwa bado halijatatuliwa kikamilifu.

BBC
Intaneti yasababisha kufungwa kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Intaneti yasababisha kufungwa kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Reviewed by Zero Degree on 5/14/2024 04:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.