Loading...

Mabadiliko ya Katiba yazua mjadala DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatarajia kuanza kufanya majadiliano kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi huku baadhi ya Wanasiasa wakiona ni njia ya Rais Felix Tshisekedi kutaka kusalia Madarakani kwa muda mrefu.

Kauli za Rais wa Congo wakati wa ziara yake barani Ulaya zimeibua mjadala baada ya kusema kuwa “Msinifanye dikteta kabla ya kuongeza, mtazamo huu sio suala langu tu, bali la raia kupitia wawakilishi wao katika Bunge la taifa.”

Kwa upande wa kambi ya Moïse Katumbi pia imetangaza kwamba mabadiliko ya Katiba ni mstari mwekundu na jukumu lao katika Bunge ni kuzuia jaribio lolote la kurekebisha Katiba.

Mashirikia ya kiraia yameonya kuwa mabadiliko ya Katiba yanaweza kuchochea vurugu zaidi nchini humo na kuitaka Serikali kujikita katika kutatua mzozo uliopo Kaskazini mwa DRC.
Mabadiliko ya Katiba yazua mjadala DRC Mabadiliko ya Katiba yazua mjadala DRC Reviewed by Zero Degree on 5/06/2024 02:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.