Tangu Rais Samia aingie madarakani kuna ahueni ya demokrasia - Prof. Lipumba
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahimu Lipumba amewataka Watanzania kuwa vinara katika ujenzi wa demokrasia ili kuepuka bakora zilizotokea miaka michache iliyopita chini ya utawala wa Rais John Magufuli.
Lipumba ametoa kauli hiyo leo Alhamis Unguja, Zanzibar kunakofanyika Mkutano wa kidemokrasia kwa mwaka 2024 ambapo amesema bakora hiyo haikuwachapa wapinzani pekee bali pia iliwagusa wanachama na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Chini ya utawala wa Rais Magufuli aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021 kwa ugonjwa moyo jijini Dar es Salaam, vyama vya siasa vilizuiwa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani kwa madai kuwa serikali ilitaka ipate muda mrefu wa kuwahudumia wananchi.
Katika mkutano huo, Lipumba amesema demokrasia ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli hivyo yoyote anayekwenda tofauti hapaswi kuchekewa wala kuonewa aibu.
“Ingawa baadhi ya watu husema udikteta huleta maendeleo lakini ukweli watu wanapokuwa huru hushiriki kikamilifu katika ujenzi wa demokrasia, ukweli miaka michache iliyopita tulipata bakora kweli kweli maana hata kukaa kwenye mikutano ya aina hii haikuwa rahisi kukaa, sasa tusirejee tena huko tukuze demokrasia” amesema.
Profesa Lipumba amesema kwa muda wa miaka 18 demokrasia duniani imeporomoka ambapo kwa mwaka 2003 Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 66 lakini ilipofika 2021 tulifikia nafasi ya 34.
“Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani mwaka 2021 angalau kuna ahueni ya demokrasia na sisi (CUF) tulisema akiendelea vizuri katika uongozi wake angalau apate tuzo la Mo Ibrahim lakini kwa hali inavyokwenda bado naona kunasuasua” amesema.

Amesema mkutano ulioitishwa na Baraza la Vyama vya Siasa mwaka juzi walikubaliana kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi na mwisho wake kikaundwa Kikosi Kazi ambacho kilitoa mapendekezo kadhaa ya kuboresha demokrasia.
“Hata sisi TCD tuliopeleka mapendekezo juu ya Katiba na hata pale tulipoona kuwa Katiba haiwezi kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025 tulipendekeza baadhi ya mambo ikiwemo namna ya Tume Huru ya Uchaguzi itakavyokuwa” amesema.
“Tulitaka yafanyike mabadiliko madogo katika Katiba ambayo ni matokeo ya urais yahojiwe mahakamani, mshindi wa urais apatikane kwa kushinda asilimia 50+1 na mgombea binafsi aruhusiwe, serikali imepeleka bungeni marekebisho ya sheria na kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa ambayo kimsingi inaonekana kama danganya toto,” amesema.
“Wajumbe wote wa Tume Huru wameshachaguliwa na hawataweza kuondolewa mpaka wamalize muda wao wa uongozi utakapokamilika hivyo, matumaini Tume Huru kuundwa upya ni kama danganya toto kwa kuwa hao hawataguswa mpaka watakapomaliza miaka mitano ambayo itakuwa baada ya uchaguzi mkuu wa 2025” amesema.
Hata hivyo, Profesa Lipumba amesema kuwa Watanzania hawana sababu ya kukata tamaa katika kupambania demokrasia kwani isipokuwapo wanaoathirika ni wao wenyewe.
“Tukipigania demokrasia bila kujali itikadi tulizonazo tutafanya maisha yetu yawe mazuri na kupiga hatua zaidi, tuitengeneze Tanzania yetu si kwa hofu,” amesema.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Reviewed by Zero Degree
on
5/16/2024 11:05:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
5/16/2024 11:05:00 AM
Rating: