Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 17 Mei, 2024


Klabu ya Napoli wanavutiwa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza, Mason Greenwood, 22 ambaye yuko Getafe kwa mkopo kutoka Manchester United, lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus ikiwa wanataka kumsajili mchezaji huyo mwenye. (Corriere dello Sport)

Atletico Madrid pia wanataka kumsajili Greenwood. (Star)

Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel anataka klabu hiyo kumhakikishia kwamba itamleta kiungo mkabaji na mchezaji nyota katika majira ya joto kabla hajajitolea kubadili mawazo yake na kusalia na kikosi hicho cha Bundesliga hadi mwisho wa msimu huu, lengo likiwa Bruno Fernandes, 29, wa Manchester United. (Independent)

Hamu ya Real Madrid kumnunua beki wa Canada Alphonso Davies, 23, ambaye kandarasi yake na Bayern Munich inakamilika msimu wa joto wa 2025 imefifia. (COPE).

Klabu ya Napoli wanamtafuta mshambuliaji wa Atletico Madrid, Samu Omorodion, 20, ambaye amekuwa Alaves kwa mkopo msimu huu, kama mbadala wa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25. (Sky Sports Italy).

Mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino anaungwa mkono na watu mashuhuri katika klabu hiyo kabla ya tathmini ya mwisho wa msimu utakaoamua mustakabali wake Stamford Bridge. (Guardian)

Kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher hana nia ya kuhamia Newcastle United, ambao kwa muda mrefu wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Real Madrid wanatazamiwa kuwapa Espanyol euro 1.5m ili kumbakisha mshambuliaji wa Uhispania Joselu, 34, kwa mkopo kabla ya kuamua iwapo watammpa mkataba wa kudumu msimu huu wa joto. (Sport)


Kiungo wa kati wa Aston Villa Mbrazil Philippe Coutinho, 31, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Al-Duhail SC ya Qatar, anaweza kujiunga na timu yake ya zamani ya Vasco da Gama kwa mkataba wa mkopo na kulazimika kuinunua kwa £5m. (TNT Sports)

Juventus wanatafakari iwapo watamfukuza meneja Massimiliano Allegri, licha ya kunyanyua taji lao kuu la kwanza katika kipindi cha miaka mitatu kwa ushindi katika fainali ya Coppa Italia siku ya Jumatano. (Sky Italia)

Klabu ya Juventus wamempa Thiago Motta wa Bologna mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Massimiliano Allegri kama kocha wao mpya. (Fabrizio Romano)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 17 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 17 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/17/2024 07:37:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.