Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 11 Mei, 2024
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25, atakuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi Real Madrid ikiwa atasaini klabu hiyo baada ya kuondoka Paris Saint-Germain. (RMCsport)
Mustakabali wa kiungo wa kati wa Uingereza Jordan Henderson mwenye umri wa miaka 33 katika klabu ya Ajax umetiwa shaka baada ya timu hiyo ya Uholanzi kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa msimu wa pili mfululizo. (Athletic)
Kuondoka kwa Mbappe kutaokoa PSG €220m (£189m) licha ya mshambuliaji huyo kuondoka kwa uhamisho huru. (Sky Sports)
Liverpool wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Algeria mwenye umri wa miaka 24 Mohamed Amoura kutoka Union Saint-Giloise. (TEAMtalk)
Ripoti zinazomuhusisha kiungo wa kati wa Newcastle Bruno Guimaraes na kuhamia Paris Saint-Germain msimu huu sio sahihi na Timu hiyo ya Ufaransa haina nia ya kumsajili Mbrazil huyo.
Meneja Mholanzi Arne Slot anatazamiwa kuhamia katika nyumba ya sasa ya Jurgen Klopp iliyoko Formby atakapomrithi Mjerumani huyo ukufunzi wa Liverpool. (Mirror)
Mazungumzo kuhusu mkataba mpya kati ya klabu ya Barcelona na kiungo wao wa kati Mhispania Marc Casado mwenye umri wa miaka 20 yamekuwa yakiendelea tangu mwezi Aprili. (Fabrizio Romano)
Bayern Munich wameanza mazungumzo na aliyekuwa kocha wao mkuu Hansi Flick kuhusu kurejea kwenye uongozi na kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel. (Sky Germany)
Barca wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa klabu ya Arsenal na Juventus kuingia mkataba na klabu ya Real Sociedad kumnunua kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Uhispania Martin Zubimendi, 25. (Mundo Deportivo)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 11 Mei, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
5/11/2024 09:35:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
5/11/2024 09:35:00 AM
Rating:

.jpeg)
.jpeg)