Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 5 Mei, 2024

Darwin Nunez, 24

Mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay Darwin Nunez, 24, analengwa na Barcelona msimu huu kama mbadala wa mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 35. (Sun).

Man United wanasubiri ofa kwa winga wa Brazil Antony, 24, huku wakitafuta nafasi katika kikosi chao kumnunua kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa na Crystal Palace aliyezaliwa Uingereza Michael Olise, 22. (Rudy Galetti).

Klabu ya Arsenal wana makubaliano ya kufanya mazungumzo na Brentford kukamilisha usajili wa kudumu wa mlinda lango kutoka taifa la Uhispania David Raya, 28, msimu huu kwa pauni milioni 27. (Fabrizio Romano)

Beki wa Uingereza Jarell Quansah, 21, yuko mbioni kupata kandarasi mpya ya muda mrefu baada ya kuonyesha kiwango kizuri msimu wake akiwa Liverpool.

Liverpool wana matumaini kuwa meneja msaidizi Pep Lijnders, ambaye anatazamiwa kuondoka msimu huu pamoja na meneja Jurgen Klopp, watarejea Anfield siku zijazo. (Mirror)

Klabu ya Manchester United inanuia kumtumia mlinzi wa Uingereza Harry Maguire, 31, kama chambo cha kuwashawishi Everton kumuuza mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, msimu huu. (Star)

Mkufunzi wa Palmeiras Abel Ferreira anataka rais wa klabu Leila Pereira kuzuia kuuzwa kwa winga wa Brazil Estevao Willian mwenye umri wa miaka 17 kwa Chelsea, ambao wameweka mezani ofa ya euro 55m (£47m). (Goal)

Kocha wa zamani wa Chelsea Graham Potter yuko katika kinyang'anyiro cha kuwa meneja wa Ajax baada ya mabingwa hao mara nne wa Uropa kukata tamaa ya kurejea tena kwa Ten Hag wa Manchester United. (De Telegraaf)

Getafe wameanza mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba mwingine wa mkopo kwa mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22. (Subscription Required)

Meneja wa Man United Eric ten Hag

Meneja wa klabu ya Manchester United Erik ten Hag ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel anayeondoka katika klabu ya Bayern Munich. (Falk Christian)

Mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 24, anavutiwa na Arsenal huku Mikel Arteta akijaribu kuimarisha safu yake ya ushambuliaji. (Tuttosport)

Klabu ya Inter Milan wako tayari kumenyana na Manchester United pamoja na Arsenal katika kinyang'anyiro cha kuwania msajili mshambuliaji wa klabu ya Bologna, raia wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 22. ( 90 min)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 5 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 5 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/05/2024 09:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.