Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 6 Mei, 2024

Gabriel Jesus, 27

Arsenal wako tayari kusikiliza ofa za kumuuza mshambuliaji wa Brazil, Gabriel Jesus, 27, msimu huu wa joto.

Matumaini ya kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips kuungana tena na Leeds United msimu huu wa joto yanategemea timu hiyo ya Elland Road kupata nafasi ya kurejea Ligi Kuu ya Uingereza.

Kocha anayeondoka wa Bayern Munich Thomas Tuchel ndiye anayeongoza kuwania nafasi ya meneja ajaye wa Manchester United huku klabu hiyo ya Ligi ya Premia iikilenga kuiziba nafasi ya Erik ten Hag. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey, 30, na Jesus wanasemekana kuwa kwenye rada za vilabu kadhaa nchini Saudi Arabia huku kandarasi za kiasi kikubwa cha fedha zikiandaliwa kwa wachezaji hao wawili wa Arsenal. (Express)

Mustakabali wa mshambuliaji wa Newcastle Callum Wilson bado haujulikani huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 32 akihusishwa na uwezekano wa kuondoka St James' Park. (Mirror)

Jadon Sancho, 24

Borussia Dortmund wanataka kusalia na winga wa England Jadon Sancho, 24, kwa mkopo msimu ujao, lakini uhamisho wa kudumu kutoka Manchester United kwa sasa hauwezekani na gharama yake ni ya juu kwa klabu hiyo ya Ujerumani. (Sky Sport Ujerumani)

Manchester United wanatumai kupata pauni milioni 100 kwa kumuuza mshambuliaji Sancho na Muingereza Mason Greenwood, 22, msimu huu wa joto. (Give Me Sport)

Mshambulizi wa Stuttgart kutoka Guinea Serhou Guirassy, ​​28, ameonekana kulengwa na Arsenal huku Mikel Arteta akijaribu kuimarisha safu yake ya ushambuliaji. (Fichajes)

Aston Villa wanakaribia kumsajili beki wa Atletico Madrid Mario Hermoso, 28. (AS)

AC Milan wako tayari kufikiria kumsajili mshambuliaji wa Canada Jonathan David, 24, kutoka Lille katika dirisha la usajili la kipindi cha majira ya joto (Calciomercato)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 6 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 6 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/06/2024 11:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.