Loading...

'Nime-imiss' mno Siku ya Mwananchi - Haji Manara


Aliyekuwa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amefunguka kuwa adhabu yake aliopewa na Shirikisho la Soka Tanzania chini ya kamati ya Maadili kutokana na makosa ya kinidhamu, ikikaribia kufika ukingoni.

Julai 2022, Manara alifungiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya Tsh milion 10.

“Tarehe 20 July Inshaallah adhabu yangu itakuwa imeisha kwa mujibu wa Judgement yao, ni chini ya mwezi mmoja toka tarehe ya leo.

“Nina hamu kubwa ya kuja kukamilisha Project flan kwa ushirikiano na wenzangu ndani ya Young Africans walau kwa mwaka mmoja au ziada kidogo”.

“Lakini nime-miss mno uwepo wangu kwenye Siku ya Mwananchi kiufupi mimi mwenyewe nime-jimiss kutokuwepo kwangu kwenye Holiday yetu.” - alisema Haji Manara.
'Nime-imiss' mno Siku ya Mwananchi - Haji Manara 'Nime-imiss' mno Siku ya Mwananchi - Haji Manara Reviewed by Zero Degree on 6/25/2024 11:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.